Wakati watu zaidi ya 1,000 wanaripotiwa kufa kutokana na ugonjwa wa Ebola katika nchi za afrika magharibi, hadi sasa serikali kupitia wizara ya afya na usatawi wa jamii haijachukua hatua zozote za tahadhali hasa kwa kutoa vifaa vya kujikinga na kutambua dalili za ugonjwa huo katika mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari.
Uchunguzi katika mpaka huo wa Sirari ambao unatumika kuingiza wageni kutoka nchi mbalimbali kupitia nchini Kenya na Uganda umebaini kuwa tangu kuibuka kwa ugonjwa huo mwezi mmoja ulipita katika nchi za afrika magharibi, serikali haikuchukua tahadhali yoyote ya kujihami na ugonjwa huo kwa kushindwa ya kusambaza vifaa vya utambuzi wa ugonjwa Ebola hatua ambayo imefanya wageni kuingia nchini bila ya kuchunguzwa.
Afisa afya mfawidhi kituo cha afya bandari ya Sirari Bw Salvatory Ludovick, amesema kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutambua ugonjwa huo, hivi sasa wanalazimika kuwakagua wageni kwa hisia hasa kulingana na mataifa wanayotoka pamoja na kuchukua taarifa zao muhimu.
Naye mganga mkuu wilaya ya Tarime Dk Charles Samson wa mjini Tarime amesema wilaya imechukua hatua za kutoa matangaza katika vituo vya afya kuzunguka mpaka wa Sirari wakati wakingojea msaada wa vifaa vya kinga na utambuzi wa ugonjwa huo kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii, huku baadhi ya wananchi katika mpaka wa Sirari wakiitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kujihami na ugonjwa huo hatari.
EmoticonEmoticon