Waandishi Ethiopia Mahakamani leo






Waziri Kuuu wa Ethiopia
Kesi inayowakabili waandishi wa habari na wanablogu 10, waliokamatwa nchini Ethiopia inaanza kusikilizwa leo, jijini Addis Ababa.
Tisa kati yao, wanaojulikana kama Zone 9 bloggers pamoja na mwingine aliyefunguliwa mashtaka bila mwenyewe kuwepo, wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidi ambayo wameyakanusha.
Wamekuwa wakishikiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa tangu mwezi April.
Taasisi ya kimataifa ya kulinda waandishi wa Habari CPJ imesema serikali ya Ethiopia wametumia vibaya sheria ya kupinga ugaidi kandamiza upinzani na uhuru wa habari.
Nayo mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameishutumu serikali ya Ethiopia kwa mashtaka hayo na kuitaka jamii ya kimataifa kushinikiza kuachiliwa huru kwa wa waandishi hao.
Previous
Next Post »