TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 11.08.2014.


·         MTU MMOJA MKAZI WA KAGERA JIJI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI AKIWA NA BAHNGI.

·         WAHAMIAJI HARAMU RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.



·         WATU WAWILI WAKAZI WA IPINDA WILAYA YA KYELA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKICHEZA KAMARI.


KATIKA MSAKO WA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ANNA MEDI (18) MKAZI WA KAGERA JIJI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 15 ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAMU 75.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.08.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MTAA WA KAGERA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO ULIOFANYWA KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


KATIKA MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIFAHAMIKA KWA JINA LA YOBE TAMANA (22) RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA AMEINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA/BILA KIBALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.08.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO MAENEO YA MWANJELWA, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

AIDHA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DIESTA TAMRADI (24) RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA AMEINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA/BILA KIBALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.08.2014 MAJIRA YA SAA 22:10 USIKU HUKO MAENEO YA KASUMULU, KATA YA IPINDA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MATATIZO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO [WAHAMIAJI HARAMU] ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


KATIKA MSAKO TATU:

WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SAMWEL KANYITA (30) NA 2. NICOLAUS GAUDENCE (31) WOTE WAKAZI WA IPINDA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKUTWA WAKIWA WANACHEZA KAMARI.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.08.2014 MAJIRA YA SAA 22:10 USIKU HUKO KATIKA MAENEO YA KASUMULU, KATA YA IPINDA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA KUJIHUSISHA NA MICHEZO ISIYORUHUSIWA KISHERIA KAMA VILE KAMARI ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO/MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA.

Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »