TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 13.08.2014.
·
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IDIWILI
WILAYA YA MBOZI AMEUAWA NA MWILI WAKE KUTELEKEZWA PORINI.
·
MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA
AJALI YA BARABARANI JIJINI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ANGELINA KAMZELA (29) MKAZI WA IDIWILI ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA
KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA SHINGONI, USONI NA KISOGONI NA
KISHA MWILI WAKE KUTUPWA PORINI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.08.2014
MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA IDIWILI, KATA NA TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALITOWEKA NYUMBANI KWAKE TANGU TAREHE 06.08.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI NA HAKUONEKANA HADI
HAPO JANA MWILI WAKE ULIPOKUTWA PORINI.
CHANZO CHA TUKIO
HAKIJULIKANI, HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI. MSAKO MKALI
UNAENDELEA KUWATAFUTA WALE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERAIA ZICHUKULIWE DHDI YAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA
MIGUU AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE WALA MAKAZI YAKE, UMRI KATI YA MIAKA
30-32 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO
BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.542 BBH AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
AITWAYE PEREGLIN ALEX (38) MKAZI WA KYELA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.08.2014
MAJIRA YA SAA 09:40 ASUBUHI HUKO
MAENEO YA KILIMO – UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa
na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon