Na William Mwamalanga
RAis jakaya kikwete kuchukua hatua za haraka kwa kuwafuta kazi mawaziri wote ambao katibu mkuu wa ccm bw, kinana aliwataja kuwa ni mizigo akiwemo waziri wa kilimo christopha chiza kabla ya mwaka 2015 vinginevyo CCM itavuna mabua kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi mkuu ujao kwani amesababisha hasara kubwa kwa wakulima wa zao la pamba na mahindi kote nchini kutokana na wizara yake kusambaza mbegu feki..
Kauli hiyo nzito ya aina yake imetolewa jana mji wa makambako-njombe na maaskofu na maashekhe 423 wanaohudhuria mafunzo ya uwekezaji kwenye mazingira ya amani kutoka wilaya zote nchini , ambao wamesema chma cha Mapindunzi kijiandae kisaikolojia pale ambapo sanduku la kura litahesabu sifuri kufuatiana uozo wa wizara ya kilimo na taasisi zake ambazo zinaztumia mamilioni ya fedha kila mwaka kwa kusambaza mbegu mbovu ambazo zimewasababishia wakulima umasikini mkubwa.
. W Akiongea kwa uchungu mkubwa katika kongamano hili wakulima maarufu wa zao pamba na mahindi kutoka simiyu ,Mbozi,Njombe shinyaga vijijini geita ,Sumbawanga manyara na iringa vijijini bw, Halieli Mwazembe, Paulo Mwanakatwe Samsoni Haule naJeladi Msigwa wamesema kitendo cha wizara ya kilimo kuagiza mbegu kutoka nje ya nchi ni mpango wa serikali wa makusudi wa kuua wakulima ,haingii akilini kwa serikali hii kuagiza mbegu nje wakati ndani ya nchi kuna wazalishaji wa mbegu wasio na idadi .
Askofu Devid mgaya ASkofu Saimoni Mshana, Shekhe ABdulla Masudi,falijali MUSSA walisema inasikitisha kuona pamoja na kilio kikubwa cha wakulima mwaka baada ya mwaka masikio ya serikali bado yamejaa ntaa, kila kona ya nchi jamii inalalamika juu ya hujuma za wachache lakini serikali inawakumbatia hii inamaana ccm mmeshindwa kuisimamia serikali ngoja tuwape wengine mwaka 2015 ndoa zinazofungwa mbele za Mungu na zinavunjwa itakuwa sisi na ccm ndugu na mashekhe na maaskofu kuanzia sasa wimbo wetu uwe ni kuvunja ndoa hii haramu alisisitiza shekhe massudi ambaye ni mkulima wa mahindi iringa, ambako mbegu feki zinauzwa kila kona na eneo jingine kwa mbegu feki kuwa ni maduka yote ya mawakala wa mbegu jijini mbeya vitongoji vyake vyake, mbalizi , mlowo tunduma mkoani mbeya na makambako mkoani njombe.
.
Akifichua siri ya maandalizi ya mbegu hizo mbovu matalaamu wa mbegu kutoka wizara ya kilimo ambaye hakuta jina litajwa hadharani amesema mbegu zote zinazo ingizwa nchini kutoka zimbabwe na,kenya ni mbovu hazifai hazina ubora wowote ni mradi wa wa kubwa pale wizarani kwani zinazalishwa na watu wasio na uwezo na utalamu wowote huku wakilipwa mamilioni ya fedha wakati kuna taasisi kama JKT na Magereza ambazo pamoja kuzalisha mbegu bora lakini hawa lipwi kwa wakati na mbegu zao hazisambazwi kwa wakulima.
Mtaalamu huyo ambaye amewataka Maaskofu wachungaji na Mshekhe kwenda vijijini mkajionee tabu na mateso makubwa wanayopata wakulima kutokana na kuuziwa mbegu mbovu ambazo huziotesha kwa gharama kubwa ya mbolea huku wakiambulia mavuno duni na kushindwa kabisa kuwapeleka watoto wao kwenye shule za maana kama wanazowapeleka hawa mafisadi watoto wao.
,Amesema kama serikali inamaanisha maana ya kilimo kwanza hainabudi kuziwezesha taasisi za utafiti wa kilimo kama taasisi ya Uyole iliyopo Mkoani Mbeya ili izalishe mbegu bora badala ya kuwapatia watu binafsi ambao wanagawa mbegu zilizo kwisha muda wake kwa kutafuta faida.
Kwa upande wake mmoja wamawakala wanaosambaza mbegu mkoani mbeya na njombe bw, atanasi Mussa amekiri kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwa wasambazaji wa mbegu hizo kwani kwa kiasi kikubwa wanashirikiana na baadhi ya wakurugenzi wakuu wa wizara ya kilimo ndiyo maana hakuna ufuatiliaji wowote ,mbegu za mwaka juzi zitasambazwa mwaka huu wa 2014/15 je hizo ni mbegu? kinachofanywa ni kupaka rangi mpya na dawa kwenye mbegu za zamani.
Kufuatia taarifa hiyo MAASKOFU NA MASHEKHE waliamua Mwenyekiti wa kongamano hilo Askofu William Mwamalanga wa Kanisa la kiinjili la kipentekoste Nchini Mchungaji William Mwamalanga alimpigie simu Mkurungenzi Mkuu wa ASA dr f,mizambwa na kumhoji kama anazo taarifa za taasisi yake kusambaza mbegu mbovu za mahindi kwa wakulima wa mikoa ya nyanda juu kusini yaani rukwa ,mbeya njombe,iringa na ruvuma ambaye alikiri kuwepo na kuzagaa mbegu feki nchini lakini akakanusha kuwa mbegu mbovu hazitokani na ASA, hata sisi asa tunaasirika sana uwepo mbegu hizo feki huku akirusha kombora kwa katibu Mkuu wa wizara ya kilimo na waziri wake ambao wanapaswa kudhibiti kuzagaa kwa mbegu hizo na siyo mimi,tuna taarifa kuzaga kwa mbegu mbovu mikoani lakini siyo jukumu langu mimi kuthibiti kazi hiyo muulizeni katibu mkuu.
DR Mizambwa aliitaja kampuni ya seedco kuwa imetajwa mara nyingi kuwa inazasambaza mbegu bovu lakini mwenye kuithibiti siyo mimi ni katibu mkuu na mthibiti mkuu wa mbegu ambao ndiyo wanayasajili makampuni hayo nendeni kwa waziri na katibu mkuu hao ndiyo wahusika wakuu kwa hayo yote alisema mizambwa
Baadaye viongozi hao wa dini walio onyesha kukerwa kwa uozo huo waliamua kumtafuta Mthibitii Mkuu wa mbegu nchini dr, HAMISI MTUENZI ambaye alikiri kuwepo kwa utitiri wa mbegu feki zinazosambazwa ovyo mikoani lakini tatizo hili linasababishwa na sheria na 18 ya mwaka 2013 na kanuni zake za mwaka 2007 ambazo zinampa nguvu mkurungezi wa mazao ndani ya wizara kutoa vibali vya kuingiza mbegu kutoka kutoka nje ya nchi hivyo siyo rahisi kwa mdhibiti wa mbegu kujua mbegu mbovu hapa tatizo ni sheria hii WAZEE WANGU TATIZO LA MBEGU HAPA KWETU NI SHERIA MBOVU.
Hata hivyo dr MTUENZI amewataka viongozi wa dini kupigia kelele sheria na kanuni hizo kwani hivi sasa mbegu nyingi zinaingizwa kutoka zimbabwe ,kenya na kwingineko hivyo bila kuwa na sheria madhubutu kilimo chetu kitakufa kutokana na mambegu mabovu yanayoingia hapa kwetu hii ikiwa ni pamoja utaratibu mbovu wa kuajiri wazalishaji mbegu wasio na uwezo wowote ;
alikri kuwa wakulima babati ambao walibaini mbegu feki za mahindi namba 513 ambazo zilikataa kuota na baada ya utafiti iligundulika zilisambaz na kampuni ya seedco ambao pia walikiri kuwa ni mbegu zao na wakakubali kufidia wakulima,ameutaja Mkoa wa Arusha kuwa unaongoza kwa makampuni mengi feki hivyo la muhimu nawaomba makampuni yote ya mbegu, mawakala na wakulima tushirikiane kupambana na uovu huo kwa kubadili sheria ya mbegu hatuna sababu yoyote kuagiza mbegu za nafaka kutoka nje ni aibu.
kongamano hili la siku wiki moja limeitishwa na kamati ya umoja wa maadili na haki za jamii kwa viongozi wa dini wataaluma na linashirikisha viongozi wa dini zote walio na taaluma mbalimbali kwa lengo la kujenga mkakati wa amani ya nchi na kufichua vikwazo vya mafanikio kwa jamii ya watanzania . ,,,mwisho
EmoticonEmoticon