MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA UDONGO.





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.08.2014.

·         MTOTO MDOGO MWENYE UMRI WA KATI YA MIAKA 03-04 AFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI MBOZI.


·         MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MIWILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KATIKA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI.

·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA UDONGO.

·         WATU WAWILI WAKAZI WA KIWIRA ROAD WILAYA YA RUNGWE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA BHANGI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:


MTOTO MDOGO MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 03 – 04 ALIYETAMBULIKA KWA JINA MOJA LA JACK AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 140 BCU AINA YA SUZUKI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA ELIUD KALINGA (54) MCHUNGAJI WA KANISA LA KKKT – TUNDUMA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.08.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO MAENEO YA VWAWA SEKONDARI, KATA YA NDALAMBO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI YA VWAWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.




KATIKA TUKIO LA PILI:


MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MIWILI (02) ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FROLA MLINGO ALIKUTWA AMEKUFA MAJI KWENYE BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.08.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA MAHANGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA KIFO CHAKE NI KUZIDIWA NA MAJI YA BWAWA HILO WAKATI AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA ILI KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.



KATIKA TUKIO LA TATU:


MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHNUYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASANGILWISYE MWAISANILA (21) ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA UDONGO WA KUFYATULIA TOFALI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.08.2014 MAJIRA YA SAA 15:45 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIANGUKIWA NA KUFUNIKWA NA KIFUSI HICHO WAKATI AKICHIMBA UDONGO KATIKA ENEO HILO.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI KATIKA SHUGHULI ZAO HASA KWA KUCHUKUA TAHADHARI ILI KUEPUKA MATATIZO.


TAARIFA ZA MISAKO:


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. JAMSE MBILINYI (27) NA 2. AMBWENE SANGA (25) WOTE WAKAZI WA KIWIRA ROAD WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA KWENYE MFUKO WA RAMBO.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 12.08.2014 MAJIRA YA SAA 19:40 JIONI HUKO KATIKA ENEO LA KIWIRA ROAD, KATA YA KAWETERE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WATUMIAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA NI KINYUME CHA SHERIA.

Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »