TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 06.08.2014.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA LUPEMBE WAPATAO 93 KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO.
·
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA
BARABARANI WILAYANI RUNGWE.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU SITA [06] KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA VITU VIDHANIWAVYO KUWA NI DAWA ZA
KULEVYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WANAKIJIJI WA KIJIJI CHA LUPEMBE WILAYANI KYELA
WAPATAO 93 KATI YA WANAKIJIJI 150 WALIOVAMIA SHULE YA SEKONDARI MWIGO
WAKIWA NA SILAHA MBALIMBALI ZA JADI WAKIWATAKA WAALIMU NA WANAFUNZI WA SHULE
HIYO WAONDOKE KATIKA ENEO HILO KWA MADAI KUWA NI MALI YA KIJIJI CHAO NA SI MALI
YA SHULE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 05.08.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA LUPEMBE, KATA YA IKIMBA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA
MBEYA. CHANZO CHA FUJO HIZO NI MGOGORO WA MPAKA WA SHULE HIYO NA ENEO HILO LA
KIJIJI.
KUTOKANA NA FUJO
HIZO, GWAMAKA ADAM (32) MKAZI WA KIJIJI CHA LUPEMBE NA
WENZAKE 92 WAMEKAMATWA, KATI YAO WANAUME NI 60 NA WANAWAKE 33. WATUHUMIWA WANAHOJIWA NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO
KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
JAMII KUFUATA SHERIA KATIKA KUDAI HAKI ZAO KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI
KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA
MIGUU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VICTOR
MODEST (17) MKAZI WA USHIRIKA
WILAYANI RUNGWE ALIGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.125 CBD AINA YA SHINEREY ILIYOKUWA
IKIENDESHWA NA FESTO STANLEY (19) MKAZI WA USHIRIKA NA KUFARIKI
DUNIA MNAMO TAREHE 05.08.2014 AKIWA
ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO
ILITOKEA MNAMO TAREHE 04.08.2014
MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO ENEO
LA USHIRIKA, KATA YA MPUGUSU, TARAFA YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA
MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA
[06] KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA KETE
06 ZINAZODHANIWA KUWA NI DAWA ZA KULEVYA.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 05.08.2014
MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO
UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA KATIKA MAENEO HAYO.
WATUHUMIWA HAO
NI PAMOJA NA 1. FIKIRI KONSO (33)
MKAZI WA MBALIZI 2. CHARLES GERVAS (26) MKAZI WA MBALIZI 3. BONIFACE BAWAGILE (27) MKAZI WA SAE 4. ERNEST MWANGOMOLE (25)
MKAZI WA SAE 5. MOSES ARON (18) MKAZI WA UYOLE NA 6. ROBERT JACKSON (23) MKAZI WA UYOLE. WATUHUMIWA HAO WALIBAINIKA KUWA NA KETE HIZO
BAADA YA KUPEKULIWA KWENYE NGUO NA MIILI YAO, UPELELEZI ZAIDI TUKIO HILI
UNAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU ZA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII/WANANCHI
KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA MTANDAO WA UUZAJI/USAMBAZAJI WA
DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na kutolewa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon