WAUMINI wapatao 30 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni leo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hadharani katika Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A” Wilaya ya Kionondoni.Katika kesi hiyo iliyounguruma kwa muda wa saa mbilli imeelezwa kuwa Julai 20 mwaka huu katika kanisa hilo lililopo eneo la Mwananyamala Msisiri ‘A’ waumini hao kwa pamoja walifanya fujo zilizosababisha kuhatarisha amani.
Kesi hiyo iliyosomwa na mwendesha mashitaka wa serikali, Credo Rugajo mbele hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo Boniphace Lihamwike, ilidaiwa kuwa Julai 20 waumini walianzisha mzozo uliosababisha waumini kupigana na kusababaisha askari polisi kutumia nguvu kubwa kutuliza fujo hizo ikiwa ni pamoja na kutumia mabomu ya machozi.
Baada ya kusikiliza kesi pande zote mbili, Hakimu Lihamwike alisema dhamana iko wazi kwa kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja anayeaminika na shilingi milioni moja kimaandishi kwa kila mmoja.
EmoticonEmoticon