UJUMBE WA TAJI LIUNDI KWA HATERS WA DIAMONDZ PLATINUMZ





HELLO HATERS! 
Psst, pssst, samahani kidogo! Oya! Wewe! Hater! Hater! Yes, ndio ni wewe hapo…samahani. 
Hali gani ndugu? Naomba nivute sikio lako! Je wewe ndo yule Supremo Hater? Usishangae, hatufahamiani haswa, na kusema ukweli na mimi nimekuhisi tu, nilivyoita ukasimama basi nimepata nguvu ya kusema nawe.
Dah, nimefurahi kupata wasaa nawe, hivi yaani naturally unajikuta unahate tu! Very unique! Ni kipaji labda…Basi nivumilie mwenzio nina kaujumbe kidogo nimefikiria. 
Kwanza kabisa naomba nikiri watu wa aina yako mimi nawasikia tu. Nawasomaga zaidi kwenye Instagram, sina experience nanyi kuubwaa kihivyo kwahiyo nipe nafasi niseme yangu kisha utavimba upendavyo, sawa?
Kuna huyu kijana anaitwa Diamondz Platinumz…nakuona unakunja uso. Inaelekea humzimikii kabisa. Hebu tuanzie hapo. Mnafahamiana, yaani kwamba ni; nduguyo au jamaa wa karibu? Rafiki au mshikaji fulani? Ningependa kujua maana naweza kuandika vitu hapa kumbe nyie mna mahusiano kamili ambayo sisi tukiona kwa nje hatuwezi elewa. Pili, je huyu Nassib,eh..? anakujua wewe? Maana hujajibu swali langu la kwanza vizuri. Anakuita nani? Mnataniana, au?
Kwahiyo wewe ni Hater wake? Yaani aina mbadala ya mshabiki hasi? Unajua najaribu sana kuelewa hii inakuwaje?Huku kuhate huku. Hadi inakuwa kama sifa hivi. Huogopi kueleweka vibaya? Maana hebu tuangalie vitu kadhaa. Diamondz ni kijana mdogo tu Mtanzania. Maelezo ya maisha yake yamejaa mtandaoni. Kiukweli na hata wewe utakiri, kijana ana nyota na pia ana kipawa au niseme talent halisi ambayo Mwenyezi Mungu Mwenyezi pekee anaweza kumshushia mwanadamu. Au hili nalo unapinga?
Previous
Next Post »