Mbeya City Council FC (MCC FC) imepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mlezi wa Tawi la Igogwe, Adventina Mwakatumbula kilichotokea usiku wa kuamkia leo (Julai 23 mwaka huu) Jijini Mbeya.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu hasa kwa MCC FC na nchini kwa ujumla kwani, Dada Adventina enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi na kushiriki katika shughuli za timu kikamilifu.
MCC FC tunatoa pole kwa familia ya marehemu Adventina Mwakatumbula, Tawi la Igogwe, na mashabiki wote wa MCC FC na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake nyumbani kwao Uyole ya Kati. Mazishi yatafanyika kesho tarehe 25 Julai 2014 hukohuko Uyole ya Kati saa 8:00mchana.
Sisi sote ni waja wake Mola. Hakika kwake tutarejea.
EmoticonEmoticon