TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 21.07.2014.
·
MZEE WA MIAKA 70 AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA
WATU WASIOJULIKANA WILAYANI MBOZI.
·
MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO
BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
·
WATU 83 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA FUJO.
·
WATU 07 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
BIBI MMOJA WA
MIAKA 70 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MANENO WILO MKAZI WA MAHENJE ALIUAWA NA
WATU WASIOFAHAMIKA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE AKIWA
AMELALA NYUMBANI KWAKE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.07.2014
MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO ENEO
LA MAHENJE, KATA YA MYOVIZI, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU ALIKUWA AMELALA NA MJUKUU
WAKE. AIDHA CHANZO CHA TUKIO BADO KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA MAPEMA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA
MIGUU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SAIDI
HASANI (30) AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.669 CFH AINA YA TOYOTA RAV4 LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA AITWAYE GEOFREY SAMWEL (46) MKAZI WA MABONDE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.07.2014
MAJIRA YA SAA 13:45 MCHANA HUKO ENEO LA KIBISI, KATA YA
KYIMO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA
MBEYA/TUKUYU. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO
KITUONI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA
MAKINI IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING]
ILI KUEPUKA AJALI.
KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 83
KATI YAO WANAWAKE 33 NA WANAUME 50 KWA KOSA LA KUFANYA FUJO BAADA YA KUTOKEA
HALI YA KUTOELEWANA KATI YA WATU WA KITONGOJI CHA KAPUGI NA KITONGOJI CHA
MATEMA WILAYANI KYELA.
INADAIWA KUWA
WATU WA KITONGOJI CHA KAPUGI [WAKULIMA] WALIWASHAMBULIA WATU WA MATEMA
[WAFUGAJI] KWA KUWAZUIA WASIPITISHE MIFUGO YAO KWENDA ENEO LA MALISHO AMBALO
WANATAKA WALITUMIE KWA KILIMO.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.07.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA KAPUGI, KIJIJI CHA MPANDA, KATA YA LUSUNGO, TARAFA YA
NTEBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
AIDHA KATIKA
TUKIO HILO WATU WAWILI WALIJERUHIWA 1.
JOB MWAKILA (32) MKAZI WA MATEMA
AMBAYE AMEVUNJIKA MKONO WA KULIA NA 2.
AYOUB MBOKA NAE ALIJERUHIWA MKONO WA
KUSHOTO, WOTE WAMEPATIWA MATIBABU.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTATUA MIGOGORO YAO
KWA NJIA YA AMANI YAANI KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA ILI
KUEPUKA MADHARA YANAYOEPUKIKA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
WATU WANNE
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUPATIKANA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA TANO [05]
KATIKA GALONI. WATUHUMIWA HAO NI 1. 1. KANALONA
MWAKANDULU (38) MKAZI WA KIJIJI CHA SYUKULA 2. BULA MOSES (30) MKAZI
WA SYUKULA 3. BOMKE ANYIMIKE (20) MKAZI WA SIKOTA NA 4. MASHAKA MAPAMBA (15) MKAZI WA SIKOTA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.07.2014
MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA ILOLO, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
WATU WATATU
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
UJAZO WA LITA TANO [05] KATIKA
GALONI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1.
NASSA LEORNAD (45) MKAZI WA
KIWIRA 2. JOEL TALALAMO (24) MKAZI WA ISAKA NA 3. YUSUPH HEZRON (26) MKAZI WA ISAKA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.07.2014
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MPANDAPANDA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
N. MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWAFICHUA WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA
UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HIYO ILI WAKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
Imesainiwa na :
[ROBERT MAYALA –ACP]
Kny: KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon