KICHANGA KILICHOOPOLEWA CHOONI TANGA CHATIMIZA MWEZI MMOJA



Mlezi wa kwaya ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Aloyce Gonzaga Parokia ya Mtakatifu Yohana Mbatizaji Luhanga Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Francis Mihayo, akiwakabidhi watoto wa kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Casa Della Diaia (Nyuma ya Furaha) cha Bombo Tanga, msaada wa vyakula na vitu mbalimbali walipotembelea kituo hicho.
 
Francis Mihayo akimkabidhi mlezi wa watoto wa kituo cha Casa Della Dioia  (Nyumba ya Furaha), Sister Consolata cha Bombo Tanga msaada wa vyakula na vitu mbalimbali.
Francis Mihayo akiwa amembeba mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Casa Della Dioia (Nyumba ya Furaha) wengine wakiwa  wamemzunguka.

KICHANGA kilichoopolewa kutoka chooni maeneo ya Pongwe mkoani Tanga kimetimiza mwezi mmoja sasa.

Kichanga hicho kiliopolewa na wasamalia wema na baadaye kupelekwa katika kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Casa Della Diaia (Nyuma ya Furaha) na sasa kimetimiza mwezi mmoja tangu kikabidhiwe katika kituo hicho na hali yake ya kiafya inaendelea vizuri.

Wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Aloyce Gonzaga, Parokia ya Mtakatifu Yohana Mbatizaji Luhanga Jimbo Kuu la Dar es Salaam walibahatika kutembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali wakiwa katika ziara ya kutembelea parokia tarajiwa ya Mtakatifu Yohana Mbatizaji ya Jimbo Katoliki la Chumbageni mkoani Tanga.

Kituo hicho kina jumla ya watoto 47, mtoto mkubwa akiwa na  miaka 22 na mdogo ana mwezi mmoja.

(Picha Gabriel Ng’osha/GPL)
Previous
Next Post »