Vinyago vinavyotumika na wajariamali kuonesha jinsi nguo ya kike itakavyomkaa mrembo au mwanaume vikiwa na taswira ya umbo la kike/ kiume vimezua hisia tofauti Iraq na Syria ambapo kundi la wapiganaji wenye itikadi kali limetoa amri.
Ripoti kutoka Iraq na Syria iliyochapishwa na mtandao wa Al Arabiya zinaeleza kuwa kundi hilo linalopatikana katika nchi zote mbili zinazoendeshwa kwa sheria za dini ya kiislamu limepitisha amri inayowataka wamiliki wa maduka ya nguo kufunika sura za vinyago hivyo kama ilivyo kwa wanawake halisi.
Kwa mujibu wa mtandao huo wamiliki wa maduka wameeleza kuwa wameamrishwa kufunika vinyago vyote vya kiume.
Msemaji wa kundi hilo la wapiganaji amesema kuwa amri hiyo imetolewa kwa kuzingatia sharia ya dini hiyo inayopinga vinyago vinavyoonesha maumbo ya binadamu.
EmoticonEmoticon