Tahadhari Facebook; Kubofya video ya msichana anaevua nguo zote itasaidia hackers kuteka akaunti yako

Tafiti zinaonesha kuna idadi kubwa ya watu wanaotumia Facebook hubofya zaidi picha au video zinazoonesha matukio yanayoendana na ngono ama picha chafu. Lakini imebainika kuwa baadhi ya video hizo hutumiwa na hackers kuweza kuaccess taarifa za mtumiaji na kuteka akaunti yake.
Wataalamu wa masuala ya mitandao wa Uingereza wamewatahadharisha watumiaji wa Facebook na kuwataka kuwa makini na video zinazosambaa zikionesha msichana au mwanamke (hata kama wanamfahamu) akiwa anavua nguo na kuonesha kuwa ukibofya itakupeleka Youtube kuangalia video nzima.
Wameeleza kuwa video hizo hutuma taarifa zisizotegemewa kwenye browsers kwenda kwenye flash player na kisha kuiba taarifa za siri za mtumiaji.
Previous
Next Post »