Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Husein Kandoro, alipokea vyandarua 650 toka kwa Askofu mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, |
Askofu Mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa MMRP jijini hapa. |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abasi Husein Kandoro akishukuru msaada huo kwaniaba ya Hospitali ya rufaa |
Dr. Leonard Maboko Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ya TAG ambae pia ni Mkurugenzi wa NIMR, akitoa neno kwa wageni |
Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dr. Kaimu Mku Humphrey Kihwelu akimkaribisha mkuu wa mkoa Mbeya |
KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) nchini linaadhimisha sherehe za miaka 75 tangu kuzaliwa kwake zinazofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.
Kutokana na maadhimisho hayo Jiji na Mkoa wa Mbeya utanufaika na sherehe hizo kutokana na shughuli ambazo Kanisa hilo litafanya katika siku zote za maadhimisho hayo.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Askofu Mkuu wa TAG nchini, Dk. Barnabas Mtokambali, katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa MMRP jijini hapa, alisema Sherehe hizo zitaambatana na shughuli mbali mbali.
Alisema maadhimisho hayo yatafikia kilele Julai 13, Mwaka huu katika sherehe zitakazofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dk. Jakaya Kikwete Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Askofu alisema kabla ya sherehe hizo kutakuwa na zoezi la kugawa vyandarua 8550 vyenye thamani ya shilingi 270 kwa ajili ya Hospital,Vituo vya Afya pamoja na zahanati zinazo laza wagonjwa katika Mikoa ya Mbeya, Rukwa na Njombe.
Askofu Mtokambali alisema mbali na kanisa kutoa msaada wa Kiroho kwa waumini wake lakini limeona katika kushurehekea miaka 75 ya tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa nchini ni bora wakafanya na huduma za kijamii.
Askofu Mtokambali alisema vyandarua vitagawiwa katika Hospitali 34 na vituo vya afya 83 katika mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa zoezi litakalofanyika kuanzia Julai 1 hadi julai 4, Mwaka huu.
Alisema katika mgawanyo huo vyandarua 1300 vitaenda Mkoani Rukwa katika Hospitali 3 na vituo vya afya 22, Mkoa wa Njombe vyandarua 3100 kwa ajili ya Hospitali 11 na vituo vya afya 25.
Askofu alisema Vyandarua 4150 vitabaki Mkoa wa Mbeya katika Hospitali 20 na vituo vya afya 36 ambapo kati yake Vyandarua 500 vitabaki katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Vyandarua 150 vitakua kwa ajili ya Hospitali ya Wazazi ya Meta.
Mbali na msaada wa vyandarua Askofu Mtokambali alisema pia kanisa hilo litaendesha zoezi la uchangaji damu litakalowagusa Wachungaji zaidi ya 800 hivyo kupunguza upungufu wa damu unaokikabili kituo cha damu salama Kanda ya Mbeya.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Husein Kandoro, alipokea vyandarua 650 kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya ambapo kati yake vyandarua 150 vitagawiwa katika Hospitali ya Wazazi ya Meta.
Mwisho.
Mbeya yetu
EmoticonEmoticon