Argentina Yaichapa Switzerland Nakutinga Robo Fainali


20140701-214621-78381758.jpg
Hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la dunia inazidi kupamba moto – leo hii Argentina walikuwa wanakipiga na Switzeland.Matokeo ya mchezo huo Argentina wamefanikiwa kwenda hatua ya robo fainali kwa ushindi wa 1-0.Goli la dakika za nyongeza la kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Angel Di Maria lilihitimisha mchezo huo mgumu ambao mpaka kufika dakika ya 90 milango yote ilikuwa migumu.

Argentina sasa anamsubiri mshindi wa mechi kati ya Belgium dhidi ya USA kwa ajili ya Robo fainali!
Previous
Next Post »