Video: Uingereza waendeleza vita na raisi wa FIFA, wahoji kwa nini haonyeshi umakini?


Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeendelea kumuandama raisi wa shirikisho la soka dunia FIFA Sepp Blatter, kufuatia kuianika hadharani video ambayo inamuonyesha akicheza pembezoni mwa mrembo Fernanda Lima, wakati wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo ukiendelea mjini Sao Paolo nchini Brazil.
Vyombo vya habari vimehoji umakini wa raisi wa FIFA ambae adaiwa kutojali sakata la rushwa linaloendelea duniani kote kwa madai Qatar ilitembeza mlungula kabla ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.
Taarifa hiyo inaendelea kusisitiza kwamba kulikuwa hakuna haja kwa Sepp Blatter, kufanya mzaha huo mbele ya wajumbe wa FIFA, na badala yake angeonyesha umakini na kusikitikia hali inayoendelea kuwatafuna kwa sasa.
Previous
Next Post »