TV, redio zifundishe Kiswahili watangazaji wao


Na Stephen Maina
Nimewahi kuandika kuwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza katika kuandika habari makala au katika mzungumzo rasmi ni kukidhalilisha Kiswahili.
Waandishi na wazungumzaji wa aina hii hawako makini na hawajali kuzingatia ufasaha wa Kiswahili.
Nilieleza kidogo katika makala zangu zilizopita kwamba watangazaji hasa wa redio na runinga zilizosajiliwa katika miaka ya hivi karibuni ndizo zisizotilia mkazo mafunzo ya lugha kwa wafanyakazi wao ili kuwainua kitaaluma kwa kuwaandalia semina na warsha za kuboresha taaluma yao katika fani za uandishi na utangazaji.
Nitatoa mifano michache ya makosa yanayofanywa na watangazaji wa runinga na redio. Kwa mfano utawasikia watangazaji wakisema:
Message unazopeleka ni za nani ?
I remember kwenye semina ya ndoa mambo yalikuwa safi.
Lakini a good office is well arranged
Hiyo intrastructure ni mbovu.
Lazima ufokasi kwenye future na maelezo mengine mengi.
Mifano hii michache inaonyesha jinsi tunavyoidhalilisha lugha yetu. Pamoja na hayo liko kundi jingine ambalo lina sauti kubwa katika jamii.
Kundi hili ni la wanasiasa na hasa wabunge ambao wanapojadili hoja bungeni au wanapowahutubia wananchi, jamii nzima ya Watanzania kukaa macho kufuatilia kinachozungumzwa.
Wako baadhi ya wanasiasa wanapozungumza hawako makini katika uchaguzi wa misamiati au istilahi za kutumia.

CHANZO MWANANCHI
Previous
Next Post »