Tazama Video Watoto wamchoma visu mwenzao mara 19 baada ya kuona filamu ya kutisha wazazi walezi tuwe makini na vile watoto wetu wanaangalia


Wasichana wawili wenye umri wa miaka 12, Anissa Weier na Morgan Geyser wanakabiriwa na kesi ya jaribio la kuua baada ya kumchoma visu mara 19 msichana mwenzao kwa kile kinachodaiwa kuigiza walichokiona kwenye filamu ya kutisha ya Slenderman.
CNN imeripoti kuwa maafisa wa polisi wa Marekani wameeleza kuwa wasichana hao waliangalia kwenye mtandao filamu hiyo ya kutisha inayomuonesha Slanderman akiwaua watoto, baadae nao wakaanza kupanga njama za kufanya unyama huo.
Wamesema watoto hao walipanga kutekeleza tukio hilo katika kipindi cha zaidi ya mwezi uliopita na kwamba walikuwa wakijadiliana mara kwa mara jinsi ya kutekeleza.
Wazo lao la awali ilikuwa kumfunga bandeji mdomoni  msichana huyo ambaye alikuwa rafiki yao na kisha kumchoma kisu shingoni, lakini baadae waliahirisha njia hiyo.
Mwisho wa siku wasichana hao waliamua kumdanganya msichana huyo kuwa wanacheza mchezo wa kujificha na kutafutana (hide and seek) na kumpeleka katika msitu mmoja eneo la Waukesha.
Walipokuwa huko mmoja alimshikilia ili asijitetee na mwenzake akafanya kazi ya kumchoma visu kadri awezavyo katika maeneo tofauti mwilini na kisha wakamuacha akitokwa damu na wakakimbia.
Russell Jack, mkuu wa kitengo cha polisi ameeleza kuwa muendesha baiskel mmoja ndiye aliyemuona msichana huyo kando ya barabara baada ya kujivuta kwa kutambaa huku akitokwa damu nyingi, na ndipo alipotoa taarifa.
Msichana huyo huko hospitali akipata matibabu na madaktari wameeleza kuwa hali yake inaimarika japo imeonekana visu vilisogea nchi chache karibu na moyo wake.
Previous
Next Post »