Jamhuri ya Afrika ya Kati yapiga marufuku kutumiana ujumbe wowote kwa simu za mkononi




Wakati Tanzania kukiwa na kampeni ya kukomesha tabia za kusambaza ujumbe mbaya kwa simu ya mkononi au mtandaoni tuliyoipa jina la ‘Delete Futa Kabisa’, serikali ya Jamhuri ya Afrika Magharibi imeamua kupiga marufuku kabisa kutumiana ujumbe wowote.
Uamuzi huo umekuja kutokana na sababu zilizotajwa kama ni kuhakikisha ulinzi na usalama baada ya kupitia katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja wakiwa katika vita ya kidini.
Serikali ya nchi hiyo imetoa tamko rasmi baada ya waandamanaji kufurika katika mitaa ya mji mkuu, Bangui huku wakihamasishana kupitia jumbe za simu za mkononi kufanya maandamano na mgumu mkubwa zaidi.
Waandamanaji hao wanataka serikali ya mpito ya nchi hiyo iliyoingia madarakani January mwaka huu kujihudhuru.
Vita ya kidini nchini humo ilianza mwaka jana baadaya Michel Djotodia aliyekuwa  raisi wan chi hiyo ambaye ni muumini wa dini ya kiislamu kujihuzuru na kukabidhi madaraka kwa watu wengi nchini humo ambao ni waumini wa imani ya kikristo.
Previous
Next Post »