Taasisi ya Chakula na Lishe yaelezea umuhimu wa vitamini A watoto


1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Elifatio Towo (Katikati) akieleza umuhimu wa vitamini A, Kushoto ni Afisa Lishe Mwandamizi Bi. Neema Joshua na kulia ni Afisa Mtafiti wa Sayansi ya Chakula Bi. Wessy Meghji.
2
Afisa Mtafiti wa Sayansi ya Chakula na Lishe Wessy Meghji akionesha aina ya vyakula ambavyo vinaongeza vitamini A, kushoto ni Elifatio Towo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe.
Upungufu wa vitamini na madini ni mojawapo ya matatizo makubwa ya kilishe yanayowaathiri hasa watoto na wanawake walio katika umri wa kuzaa hapa Tanzania. Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii (Demographic and Health Survey) za mwaka 2010 zinaonesha kuwa hapa Tanzania upungufu wa vitamini A unaathiri asilimia 33 au theluthi moja ya watoto walio chini ya miaka mitano na asilimia 37 au zaidi ya theluthi moja ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Upungufu wa madini chuma unaathiri asilimia 59 au zaidi ya nusu ya watoto wadogo na karibu asilimia 41 au karibu ya nusu ya akina mama wajawazito, na pia upungufu wa madini joto unakadiriwa kuathiri asilimia 7 ya Watanzania. Njia mojawapo ambayo inatumika kupunguza tatizo
Kwa kuanzia tuangalie upungufu wa vitamini A
•      Vitamini A ni mojawapo ya vitamini isiyotengenezwa na mwili na hivyo ni lazima itokane na vyakula
•      Vyakula vywenye vit A kwa wingi
–     Mboga na matunda hasa yenye rangi ya kijani na njano
–     Samaki hasa dagaa
–     Mafuta ya mawese
–     Maini
–     Viazi lishe
Sababu za Upungufu
•              Ulaji duni usiokidhi mahitaji ya Vit A mwilini
•              Unyonyeshaji watoto maziwa ya mama usiofuata kanuni (Sub optimal breastfeeding)
•              Magonjwa ya mara kwa mara
•              Utunzaji duni wa makundi husika
•              Mgawanyo mbaya wa rasilimali
Waathirika wakuu:
•      Watoto walio katika umri wa chini ya miaka mitano
•      Wanawake walio katika umri wa uzazi.
•      Asilimia 33 ya watoto walio katika umri wa chini ya miaka 5 wana upungufu wa vitamini A
•      Asilimia 37 ya akina mama walio katika umri wa kuzaa wana upungufu wa vitamini A
Madhara ya Upungufu wa vitamini A
•      Kutokuona vizuri kwenye mwanga hafifu
•      Upofu
•      Maradhi ya mara kwa mara kutokana na kupungua kwa kinga ya mwili
•      Vifo hasa vya watoto
•      Kushuka kwa elimu
•      Kupungua kwa tija
Njia zinazotumika kupambana na tatizo
•      Unyonyeshaji sahihi wa watoto
•      Ulaji wa vyakula vyenye virutubishi hasa vya vitamin A kwa wingi na vya mchanganyiko
•      Ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi (Hasa vile vyenye rangi ya kijani kibichi na njano)
•      Uongezaji virutubishi vya vitamini A kwenye vyakula (mafuta ya kula)
•      Kutoa nyongeza ya matone ya vitamini A kwa watoto walio katika umri wa miezi 6 hadi miaka mitano
Utoaji wa matone ya vitamin A
Matone ya vitamini A hutolewa  kwa watoto walio katika umri wa miezi 6 hadi miaka mitano mara mbili kwa mwaka (June na December)
Watoto wa umri wa miezi 6 hadi miezi 11 hupewa kidonge chenye IU 100,000
Watoto wa umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano hupewa kidonge chenye IU 200,000
Matone yanatolewa katika vituo vya afya na vituo vya muda hususani kwa kazi hiyo ili kuwafikia watoto wengi zaidi nia ikiwa ni kuwafikia wote.
Kwa Tanzania zoezi limekuwa likiwafikia watoto zaidi ya asilimia 80.
Wakati wa zoezi la utoaji wa matone ya vitamini A watoto wote wenye umri wa mwaka 1 hadi miaka 5 hupatiwa pia dawa ya kutibu minyoo
Changamoto Ambazo Zinafanyiwa Kazi
Baadhi ya changamoto zilizopo ni pamoja na: Mfumo wa usambazaji matone ya vitamini A ili kuhakikisha walengwa wanavipata kwa wakati.
Ukusanyaji wa takwimu za kiwango kilichofikiwa na kuwasilisha taarifa kwa wakati
Kuweza kuwafikia walengwa wote hasa maeneo ambayo ni korofi
Wazazi na walezi wanapaswa kufahamu nini? Ujumbe muhimu
Kila mzazi / mlezi wa mtoto mdogo anapaswa kufahamu umuhimu wa vitamini A kwa ukuaji, maendeleo mazuri, afya na uhai wa mtoto.Vile vile vyakula tunavyokula havikidhi mahitaji ya vitamini A kwa watoto kwani hula kiasi kidogo wakati mahitaji yao ni makubwa na hivyo ni muhimu wapatiwe matone ya vitamini A mara mbili kila mwaka. Pia wanapaswa kufahamu wakati na mahali ambapo zoezi la utoaji wa matone ya vitamini A hufanyika ili waweze kuwapeleka watoto wao kila baada ya miezi sita
Kwa mwaka huu 2014 matone ya vitamin A na dawa za minyoo zinatolewa lini
Mwaka huu wa 2014 matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo zitatolewa kwa awamu kama ifuatavyo
Awamu ya kwanza matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo zitatolewa katika halmashauri zote za Tanzania Bara katika kipindi chote cha mwezi ujao wa Juni 2014 kwa watoto wote wenye umri wa miezi 6 – 59 (vitamini A) na watoto wote wa umri wa mwaka 1 – 5 (dawa za kutibu minyoo).
Awamu pili matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo zitatolewa katika halmashauri zote za Tanzania Bara katika kipindi chote cha mwezi wa Disemba 2014 kwa watoto wote  wenye umri wa miezi 6 – 59 (vitamini A) na watoto wote wa umri wa mwaka 1 – 5 (dawa za kutibu minyoo).
Wazazi na walezi wapelekeni watoto wakapate matone ya vitamini A na dawa zaminyoo kwa ajili ya kuboresha afya na ukuaji wao kwani ni haki yao.
Wanahabari hamasisheni jamii kuwapeleka watoto walengwa wakapate matone ya vitamini A na dawa za kutibu minyoo kwa kuwafikishia ujumbe sahihi.
Previous
Next Post »