MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA RISASI KIFUANI KWA BUNDUKI/SILAHA.






TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 02.06.2014.

·         MTU MMOJA AMEKUTWA AMEUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI.


·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA RISASI KIFUANI KWA BUNDUKI/SILAHA.

·         WATU WATANO WANASHUIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA MBALIMBALI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ROBERT BUKUKU (26) MKAZI WA KIJIJI CHA IPANGA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.06.2014 MAJIRRA YA SAA 23:00 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA LUKWEGO, KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA KUVUNJA NA KUIBA KATIKA KANISA LA TAG-IBOLELO. KANDO YA MWILI WA MAREHEMU KUMEKUTWA VITU VILIVYOIBWA MALI YA KANISA HILO AMBAVYO NI PAMOJA NA GENERATOR MOJA NDOGO AINA YA BIBLA-YAMAHA, VITI 8 VYA PLASTIKI, SAA MOJA YA  UKUTANI AINA YA SAMAY, SPANA 11 ZA AINA MBALIMBALI, MKEKA MMOJA, MAUA MAWILI YA  MEZANI NA KITAMBAA KIMOJA.

AIDHA WATUHUMIWA WATANO WAMEKAMATWA 1. HEZRON MALIYABIBI (50) MCHUNGAJI –TAG-IBOLELO 2. KENEDY GWALUGANO (29) MKAZI WA LUKWEGO 3. JOEL MWAKYUSA (44) MWENYEKITI KITONGOJI CHA MASUNGWA 4. BENSON KAJUNI (48) MKAZI WA KIKOTA NA 5. KAIRO HASSAN @ MJEGE (38) MKAZI WA LUKWEGO.


KATIKA TUKIOP LA PILI:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FURAHA WILSON @ MATAKO (37) MKAZI WA KIJIJI CHA ICHENJEZYA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI KWA KUTUMIA SILAHA/BUNDUKI AINA YA S/GUN ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.  

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI KATIKA KJIJI CHA BARA KATA YA BARA TARAFA YA ITAKA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. KANDO YA MWILI WA MAREHEMU IMEKUTWA SILAHA BASTOLA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA INAYOTUMIA RISASI ZA SHORT GUN IKIWA NA RISASI MOJA KWENYE MTUTU. AIDHA KWENYE SURUALI ALIYOKUWA AMEVAA MAREHEMU IMEKUTWA RISASI MOJA YA S/GUN.

AIDHA, MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA KUBWA KIFUANI NA MGONGONI. AIDHA INADAIWA/INASEMEKANA MAREHEMU ALIKUWA NI MHALIFU SUGU NA MZOEFU. CHANZO KINACHUNGUZWA.


KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SARAH ATHUMAN (28) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AKIWA NA   POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10] KWENYE KAMBI YAKE YA  KUCHIMBIA DHAHABU.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA KASAKALAWE, KATA YA   MATUNDASI, TARAFA YA   KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

AIDHA, MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA PIA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA KILO TATU [03] KWENYE KAMBI YAKE YA KUCHIMBIA DHAHABU.

KATIKA MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAMECK ALINDA (55) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AKIWA NA   BHANGI UZITO WA KILO KUMI [10] IKIWA KATIKA KIKAPU KILICHOFUNGWA KWENYE BAISKELI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:20 JIONI KATIKA KIJIJI CHA KASAKALAWE, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA   KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA,  MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA TATU:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ANTHONY LUKAS (19) NA 2. ISAKA KALUKA (24) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IHOMBE WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 750.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA IWANGA, KATA YA IHOMBE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA/POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA KUUZA BHANGI/POMBE HARAMU YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »