MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA MPINI WA SHOKA KICHWANI KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 04.06.2014.

·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA MPINI WA SHOKA KICHWANI KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI WA UYOLE AKIWA NA NOTI BANDIA 22.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HAPIFANIA VITUS SIMFUKWE (25) MKAZI WA KIJIJI CHA TONTELA ALIUAWA KWA KUPIGWA MPINI WA SHOKA KICHWANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PAUL SILUMBE (19) MKAZI WA KIJIJI CHA TONTELA NA KISHA MWILI WAKE KUUTUPA PORINI.

MWILI WA MAREHEMU ULIONEKANA PORINI MNAMO TAREHE 03.06.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA TONTELA, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NA MAHUSIANO YA  KIMAPENZI NA MTALAKA WAKE PRISCA DOTO MDORO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANANDOA KUTATUA MATATIZO/MIGOGORO YAO KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOJITOKEZA.


KATIKA TUKIO LA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE AITWAYE AHMAD ABDALLA (20) AKIWA NA NOTI BANDIA ZIPATAZO 22 KILA MOJA IKIWA NA THAMANI YA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 220,000/=.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.06.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA KATIKA ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUTAKA KUZIWEKA FEDHA HIZO KWENYE AKAUNTI YAKE YA M-PESA. NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA BK – 4835477 NOTI 04, BP-7527147 NOTI 04, AP-5136675 NOTI 02, BU-3357146 NOTI 02, AP-5136776 NOTI 02, BU-7716837 NOTI 01, AP-5136778 NOTI 01, BU-7716833 NOTI 01, BX-8643537 NOTI 01, BU-77168391 NOTI 01, BU-77168351 NOTI 01, BU-7716836 NOTI 01 NA AP-5136778 NOTI 01. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HUSUSAN WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI NA WATEJA WANAFIKA KATIKA MAENEO YAO KWA LENGO LA KUWEKA FEDHA IKIWA NI PAMOJA NA KUHAKIKI FEDHA KABLA YA KUTOA HUDUMA. AIDHA ANAWATAKA WANANCHI KUWA WEPESI KUTOA TAARIFA PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYA MTU/WATU AMBAO HAWANA IMANI NAO KATIKA MAENEO YAO IKIWA NI PAMOJA NA MATAPELI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


Imesainiwa na:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




Previous
Next Post »