TANGAZO KWA WAANDISHI WA HABARI WOTE MKOA WA MBEYA.



Kutakuwa na ziara (picknik) ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya nchi jirani ya Malawi mwishoni mwa mwezi wa Nane mwaka huu kwa lengo la kujifunza mambo mbali mbali ya kihabari kutoka kwa wenzetu pamoja na kutembelea maeneo muhimu.

hivyo basi kutokana na umbali wa sehemu yenyewe kila atakayependa kujumuika kwenye ziara hiyo kutakuwa na mchango ambao ni nauli pamoja na fedha za chakula cha pamoja.

kila mshiriki atalazimika kuchangia fedha za kitanzania shilingi Laki mbili 200,000/= tu kwa ajili ya nauli na gharama zingine za kwenda na kurudi.

mwisho wa mchango huo ni tarehe nane mwezi wa nane mwaka huu (8/8/2014) na mchango huo uwasilishwe kwa mwenyekiti wa kamati ya Safari Brandy Nelson 0754011770 na ili kurahisisha unaruhusiwa kuchanga kidogo kidogo kuanzia 50,000/=.

ni matumaini yangu kuwa wazo hili limepokelewa na kuungwa mkono na waandishi wenzangu kwa lengo la kupanua wigo wa ufahamu katika kazi zetu.

wenu,

Venance Matinya.
Mratibu wa safari.

ukipata ujumbe huu mtaarifu na mwenzio
Previous
Next Post »