TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 09.06.2014.
·
MTU MMOJA AKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU
CHENYE NCHA KALI NA KISHA MWILI WAKE KUTUNDIKWA KWENYE MTI.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA
GARI WIALYANI RUNGWE.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WLLIAM
KABINJI (38) MKAZI WA KIJIJI CHA
MANTENGU [A] ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI
KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA SEHEMU ZA USONI
NA JUU YA JICHO LA KUSHOTO KISHA
KUNYONGWA SHINGO NA KUTUNDIKWA JUU YA
MTI AKIWA AMEFUNGWA SHINGONI KWA KUTUMIA
KITENGE.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.06.2014
MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA KATIKA
KIJIJI CHA ILEMBO, KATA YA VWAWA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MAREHEMU KUCHOMA MOTO NYUMBA TATU ZA JIRANI
ZAKE NA KUITEKETEZA KABISA NYUMBA YA ELIAS MWAMLIMA (32) MKAZI WA KIJIJI CHA
MANTENGU [A] TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA SAA 21:30 USIKU NA KUTOROKA.
JITIHADA ZA
KUWASAKA NA KUWAKAMATA WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AMBAO NI MAJIRANI WANAOFAHAMIKA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTEMBEA KWA
MIGUU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA EZEKIEL
KYANDO (72) MKAZI WA BAGAMOYO
AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU
KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.06.2014
MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI KATIKA
ENEO LA BAGAMOYO TUKUYU MJINI, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU KATIKA
BARABARA YA MBEYA/TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. UCHUNGUZI UNAONYESHA
KUWA CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
AJALI HIYO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA NONDE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SAMSON JULIUS (18) AKIWA NA BHANGI KETE 68
SAWA NA UZITO WA GRAMU 340.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 08.06.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA ENEO
LA STENDI KUU YA MABASI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA.
MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon