Mwili wa marehemu Yasin Jailan (15) aliyekata roho ndani ya wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro huku dokta akizichapa kavukavu.
Akiwa mitaani akisaka matukio, mwanahabari wetu alivutiwa waya na chanzo chetu kisha akatonywa kuwa kuna bonge la timbwili kwenye wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro ambapo alitii wito na kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri (huwa Global hatulazi damu kufika eneo la tukio).
Alipofika wodini hapo, mwandishi wetu alishuhudia mtoto akikata roho huku baba mwenye mgonjwa aliyetajwa kwa jina la Jailan Mrisho akizichapa na daktari ambaye jina halikupatikana.
Baba wa marehemu (kushoto) akilia kwa uchungu.
Alidai kuwa baada ya vipimo vya mwanaye walishauriwa kwenda kununua dawa ambazo ziliwagharimu shilingi elfu arobaini.
Alisema walipofanikiwa kupata fedha na kununua dawa hizo, daktari alidaiwa kumuuzia mgonjwa mwingine hivyo kusababisha timbwili hilo.
Dada wa marehemu naye akiwa hospitalini hapo.
Baada ya kuona hali tete huku watu wakiwa na hasira wakimlalamikia daktari huyo kwa uzembe, mwanahabari wetu alipiga simu kituo kikuu cha polisi mkoani hapa ambapo polisi wa pikipiki almaarufu kama tigo walifika na kumchukua daktari huyo kisha kumkimbiza kituoni kumnusuru na kipiga kutoka kwa watu wengine ambao walifika hospitalini hapo kuwaona wagonjwa wao.Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, John Laswai alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi baada ya kumnusuru dokta huyo ambaye kwa sasa anadunda mtaani.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mipango ya mazishi ya marehemu ilikuwa ikifanyika nyumbani kwao maeneo ya Mkuyuni mkoani hapa.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kwamba kumekuwa na vifo vingi vinavyosababishwa na madaktari ambao hawana wito wa kazi hiyo hivyo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii chini ya waziri wake, Dk. Seif Selema Rashid kuchukua hatua juu ya suala hilo.
CHANZO:IJUMAA WIKIENDA
EmoticonEmoticon