Mahakama ya Iran yamuita mwanzilishi wa Facebook kujibu tuhuma, itamuadhibu asipohudhuria



Mwanzilishi na mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg ameitwa na mahakama ya Iran kujibu tuhuma za uvunjifu wa haki za usiri/faragha na kuingilia mambo binafsi.
Maafisa wa Iran wameliambia shirika la habari la ISNA kuwa Zuckerberg anatakiwa kufika katika mahakama iliyopo jimbo la Fars ambapo kampuni yake ya Facebook na mitandao inayoimiliki kamaWhatsApp na Instagram inatuhumiwa kuvunja sheria.
Mahakama hiyo inamtaka Zuckerberg au mwanasheria wake kufika katika mahakamani na kwamba endapo hatahudhuria mitandao hiyo itafungiwa na huenda akalipishwa faini.
Wito huo unakuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu vijana sita wa Iran kukamatwa baada ya kupost video inayowaonesha wakicheza wimbo wa Pharrell Williams ‘Happy’ wakiwa juu ya paa la nyumba huko Tehran.
Imeripotiwa kuwa muongozaji wa video hiyo bado yuko rumande.
Previous
Next Post »