TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 23.05.2014.
Ø
VYUMBA KUMI
VYATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA AJALI YA
MOTO.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO
KWA KUNYWA POMBE BAADA YA MUDA.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA WATU WATATU
KWA KUKAMATWA NA SILAHA MBILI AINA YA
GOBOLE.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA KWA KUKUTWA NA BHANGI.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA KWA KUKUTWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI[GONGO].
TUKIO
LA KWANZA.
VYUMBA KUMI VYATEKETEA KWA MOTO KUTOKANA NA AJALI YA MOTO.
KIJANA MMOJA ERICK ROGERS [17] MWANAFUNZI, MKAZI WA MANGA –VETA ALIGUNDUA
KUUNGUA MOTO KWA NYUMBA YAO NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA KATIKA VYUMBA
KUMI [10] VYA NYUMBA HIYO.
TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 22.05.2014
MAJIRA YA SAA 21:50HRS USIKU HUKO KATIKA ENEO LA MANGA – VETA KATA YA ILOMBA,TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO
KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI HITILAFU YA UMEME KATIKA CHUMBA KILICHOKUWA NA MASHINE
YA KUTOTOLESHEA VIFARANGA VYA KUKU. HATA
HIVYO MOTO HUO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA
KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI,POLISI NA WANANCHI. AIDHA KATIKA TUKIO
HILO MMILIKI WA NYUMBA HIYO ROGERS
SHIPELA [56] AKIWA KATIKA HARAKA ZA KUZIMA MOTO ALIANGUKIWA NA TOFALI
MGONGONI NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI AMBAPO ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA.
THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA BADO
KUFAHAMIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI
YA MAJANGA YA MOTO.
KATIKA
MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 10 KUTOKANA NA MISAKO
MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA
KWANZA JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KUKUTWA WAKINYWA POMBE BAADA
YA MUDA KWISHA, WATUHUMIWA HAO NI 1. MATASHA ZUBERI [38],MKAZI WA MTAA WA BENK 2. VICK
MICHAEL [29]MKAZI WA MTAA WA BENK, 3. YUSUPH MWANSASU [30], MKAZI WA JUAKALI 4. NGOME
SANGA [33], MKAZI WA MWANJELWA NA 5. OLI MAULID [30],MKAZI WA MWANJELWA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 22.05.2014
MAJIRA YA SAA 23:45HRS USIKU KATIKA KILABU CHA POMBE KIITWACHO KINGANI-UYOLE
KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI
LIMEMKAMATA PETER DAIMON [25] MKAZI WA MLIMA RELI-MBALIZI AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 256.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 22.05.2014
MAJIRA YA SAA 13:30HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MSHIKAMANO, KATA YA UTENGULE-USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. TARATIBU ZINAFANYWA
ILIAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA TATU JESHI LA POLISI KWA
KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA WANYAMAPORI WA PORI LA MITUNDU-RUNGWA WALIWAKAMATA WATU WATATU WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI
MBILI AINA YA GOBOLE BILA KIBALI.
WATUHUMIWA HAO NI 1. EMANUEL CHAPA [42] 2
. MASHAKA PATRICK [39] NA 3. ABRAHAM
MWAITURO [58] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NKUNG’UNGU-LUPA WILAYA
YA CHUNYA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 21.05.2014
MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NKUNG’UNGU,KATA YA LUPA,TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI.
AIDHA KATIKA TUKIO LA NNE JESHI LA POLISI
LIMEFANIKIWA KUMKAMATA TUMPE EDWARD [28],
MKAZI WA MAPELELE AKIWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 1.5
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 22.05.2014
MAJIRA YA SAA 17:30HRS JIONI NA HUKO
KATIKA MAENEO YA DDC-MBALIZI, KATA
YA MBALIZI, TARAFA YA BONDE LA USONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI
SILAHA BILA KIBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAWINDAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA
DHIDI YAO ZICHUKULIWE MARA MOJA.
Signed by:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon