TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 24.05.2014.
Ø
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA BHANGI.
TUKIO
LA KWANZA.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA JIWE KICHWANI.
MTU MMOJA BARIKO
MWAKASISILE [40], MKAZI WA KIJIJI CHA NYELELE- BUJONDE WILAYA YA KYELA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA
KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA
WILAYA YA KYELA TAREHE 23.05.2014
MAJIRA YA SAA 16:00HRS ALASIRI.
MAREHEMU ALIPIGWA JIWE KICHWANI NA LUPAKISYO
JACOB, MKAZI WA KIJIJI HICHO. TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.05.2014
MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU HUKO KATIKA KITONGOJI CHA NYELELE, KIJIJI NA KATA YA BUJONDE TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA TUKIO HILO KINACHUNGUZWA NA
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU
YA MAHALI ALIPOKIMBILIA MTUHUMIWA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
KATIKA
MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI [02] KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO LA KWANZA
JESHI
LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA THOMAS
BENEDICTO [30], MKAZI WA MBUGANI – KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI KETE 62 ZENYE UZITO WA GRAMU 460 PAMOJA NA BHANGI AMBAYO BADO
HAIJASOKOTWA GRAM 500,YOTE IKIWA NA
UZITO WA GRAM 960.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 23.05.2014
MAJIRA YA SAA 08:30HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA KALUMBULU, KATA YA KYELA - KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI
WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI.
KATIKA
TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI LIMEMKAMATA MTU MMOJA
MWANGOTA MWANGOTA [40], MKAZI WA KIJIJI
CHA IBUNGU KYELA KWA KUKUTWA NA BHANGI KETE 70 ZENYE UZITO WA GRAMU 350.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 23.05.2014
MAJIRA YA SAA 09:45HRS ASUBUHI HUKO ENEO LA MBUGANI, KATA YA KYELA KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI
WA BHANGI NA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na
[ B.N.MASAKI – ACP ].
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon