·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MISHE YA BHANGI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA
POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
KATIKA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AITWAYE DAMISYE ABID (40) AKIWA AMEINGIA
NCHINI BILA KIBALI.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA MNAMO TAREHE 07.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30
ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA STENDI KUU KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA
YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BITON MARTIN (25) MKAZI WA KIWIRA AKIWA NA MICHE
MIWILI YA BHANGI NYUMBANI KWAKE.
MTUHUMIWA
HUO ALIKAMATWA KATIKA MTAA WA KIWIRA ROAD, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU,
WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 07.05.2014 MAJIRA YA SAA
18:30 JIONI. MTUHUMIWA NI MKULIMA WA ZAO HILO HARAMU NA TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KATIKA MSAKO WA TATU:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LAKAMATA POMBE KALI [VIROBA] AINA YA
DOUBLE PUNCH KATONI 04 NA CHARGER KATONI 06. BIDHAA HIZO
ZILIKAMATWA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA ENEO LA NJIA PANDA KASUMULU, KATA
YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA MNAMO TARHE 07.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KUTUPA MZIGO BAADA YA KUWAONA
ASKARI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO
YAO ILI UCHUNGUZI ZAIDI UFANYWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
HATARI KWA AFYA ZAO NA NI KINYUME CHA SHERIA. HALIKADHALIKA KWA WAFANYABIASHARA
KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon