TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14.05.2014.




Ø  WATU WAWILI  WAUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI  KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.


Ø  MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA SULULU NYUMBANI KWAKE.

Ø  JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA POMBE YA  MOSHI[GONGO] NA MTAMBO MMOJA.

Ø  JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NAMAMLAKA NYINGINE ZA UDHIBITI LINAWASHIKILIA WATU 15 KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA/KUUZA BIDHA BANDIA /ZILIZOKWISHA MUDA WAKE.



TUKIO LA KWANZA.

WATU WAWILI  WAUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.


WATU WAWILI,  MMOJA  ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA  DAITAN SWALE [30] NA MWENZAKE AMBAYE AMEFAHAMIKA KWA JINA MOJA MIKE MKAZI WA MTAA WA MAKUNGULU JIJINI MBEYA WALIPOTEZA MAISHA   KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO  NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI KWA  WAKITUMIA SILAHA ZA JADI  MAWE, FIMBO NA MARUNGU.TUKIO HILI LILITOKEA TAREHE 13/05/2014 MAJIRA YA SAA 08:40HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MSANGAMWELU KATA YA MSHEWE,TARAFA YA BONDE LA USONGWE. MAUTI YALIWAPATA WATU HAO BAADA YA WAO NA WENZAO WATATU KUFANYA UNYANG’ANYI BAADA YA KUTEKA GARI AINA YA FUSO T.952 AMR LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA  MUSA JOHN SIKU YA TAREHE 12/05/2014 MAJIRA YA SAA 02:30HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA MSANGAMWELU MBEYA VIJIJINI BAADA YA KUWEKA MAWE KATIKA BARABARA YA MBALIZI- MKWAJUNI AMBAPO LORI LILIPOSIMAMA ILI WATOE MAWE HAYO WALIWAWEKWA CHINI YA ULINZI NA MAJAMBAZI KUPORA SIMU ZA MIKONONI , PIKIPIKI MOJA T.682 CHT AINA YA  SANYA ILIYOKUWA NDANI YA  GARI HILO  NA FEDHA KIASI AMBACHO BADO HAKIJAFAHAMIKA, KWANI WATU HAO WALIKUWA WAMETOKA KUNUNUA MAZAO YA UFUTA.HIVYO KUTOKANA NA TUKIO HILO WALIPIGA KELELE KUOMBA MSAADA NA WANANCHI WALIJITOKEZA NA KUWEZA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WATATU AMBAO NI 1.NYOROBI MTEGO [26] MKAZI WA IGUNGA-TABORA 2. IDDI SADICK [29] 3. KITWANA LUGOYA [30] MKAZI WA ILEMI JUHUDI MBEYA AMBAO WALIPIGWA NA WANANCHI HAO NA MMOJA KUFARIKI KUTOKANA NA KIPIGO HICHO NA 02 WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

DAITAN SWALE  NA MWENZAKE WALIFANIKIWA KUKIMBIA KUTOKA KWENYE ENEO LA TUKIO LAKINI WANANCHI WALIENDELEA KUWAFUATILIA KUFANIKIWA KUWAKAMATA HUKO KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA MSANGAMWELU, TARAFA YA BONDE LA USONGWE NA KUWAPIGA NA KUPELEKEA KUPOTEZA MAISHA YAO. MAREHEMU DAITAN SWALE ILIFAHAMIKA KUWA NI JAMBAZI SUGU/HATARI AMBAE ANATUHUMA ZA UNYANGANYI WA KUTUMIA SILAHA/MAUAJI KATIKA WILAYA ZA  MAFINGA MKOA WA IRINGA NA WILAYA YA MBARALI MKOANI MBEYA.MAREHEMU NA WENZAKE WALIKUTWA NA SIMU WALIZONYANG’ANYA . MIILI YAO IPO KATIKA CHUMBA CHA MAITI HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI PINDI WANAPOWAKAMATA WATUHUMIWA KWA TUHUMA MBALIMBALI BADALA YAKE WAHAKIKISHE WANAWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ICHUKULIWE.  AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO RAI KWA JAMII HUSUSANI WAKULIMA NA WAFANYABIASHARA WA MAZAO KUEPUKA TABIA YA  KUTEMBEA/KUWEKA NDANI YA  NYUMBA   KIASI KIKUBWA CHA FEDHA  ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. PIA KAMANDA MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUKIO YA  KIHALIFU KWANI WANAHATARISHA MAISHA YAO BADALA YAKE WAPAMBANE NA UMASIKINI KWA NJIA HALALI.



TUKIO LA PILI.

MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA SULULU NYUMBANI KWAKE.

MTU MMOJA RIZIKI SIAME @ NKOTA [30] MKAZI WA KIJIJI CHA PATAMELA ALIUAWA KWA KUPIGWA SULULU UTOSINI NA MDOMONI AKIWA NYUMBANI KWAKE.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014 MAJIRA YA  SAA 04:00HRS KATIKA KITONGOJI CHA SHULENI, KIJIJI CHA PATAMELA,KATA YA  SAZA,TARAFA YA  KWIMBA WILAYA YA  CHUNYA. MAREHEMU ALIUAWA NA WATU WAWILI  AKIWA NJE NYUMBANI KWAKE AMBAO NI 1. MOLANI MWASHILINDI [27] NA 2. STEPHEN SINGOGO [25] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IGANDU, KATA YA  MSIHA WILAYA YA  MBOZI AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA  KUFANYA TUKIO HILO.

CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI  ULIOTOKEA  KATI YA  MAREHEMU NA WATUHUMIWA  KUGOMBEA PESA  ZILIZOTOKANA NA MAUZO YA DHAHABU.   

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII  KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INALETA ATHARI KUBWA KWA JAMII. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.



KATIKA MSAKO.

JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAWASHIKILIA WATU KUMI [10] KWA MAKOSA MBALIMBALI YALIYOTOKANA NA MISAKO ILIYOFANYIKA.  KATIKA TUKIO  LA KWANZA  JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA VEWA NYOTO [39]  MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA   BAADA YA  KUKAMATWA AKIWA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 60 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.

MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA  TAREHE 13.05.2014 MAJIRA YA  SAA 12:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA ILEMI,  KATA YA  ILEMI, TARAFA YA  SISIMBA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NI NA MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI KUFIKISHWA MAHAKAMANI.

KATIKA MATUKIO MENGINE  JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA NYINGINE ZA SERIKALI TRA, TFDA, TBS NA MAMLAKA YA  VIPIMO LINAWASHIKILIA WATU 15 KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA BIDHAA ZILIZOPITA MUDA WAKE, KUUZA VYAKULA AMBAVYO HAVIJASLIWA, KUPATIKANA NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI,KUPATIKANA NA POMBE KALI [VIROBA] VILIVYOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI PAMOJA NA KUUZA SIMU ZINAZODHANIWA KUWA NI BANDIA.
           
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO MAALUM ULIOHUSISHA IDARA HIZO KATIKA MAENEO MWANJELWA,SOWETO,MBALIZI, MAFIATI,ILOMBA PAMOJA NA KIWIRA NA TUKUYU WILAYA YA  RUNGWE.


MSAKO HUO ULIFANYIKA TAREHE  13.05.2014 MAJIRA  KATI YA  SAA 10;00HRS HADI SAA 14:00HRS KATIKA MAENEO HAYO. WATUHUMIWA WALIHOJIWA NA KUPEWA DHAMANA,  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI  WAHUSIKA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA  KUWA MAKINI PINDI WANAPONUNUA MAHITAJI KWA KUKAGUA BIDHAA HIZO KAMA ZINA VIWANGO VINAVYOSTAHILI AU VINA VIWANGO VINAVYOSTAHILI.


Imetolewa na:
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »