RAY C AMSAIDIA VIDEO QUEEN WA NGOMA YA NOORAH ALIYEATHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA



STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila’Ray C’amemsaidia aliyekuwa video Queen wa ngoma ya Ice Cream ya msanii wa siku nyingi wa muziki huo Noorah baada ya kuathirika na utumiaji wa madawa ya kulevya.Kupita ukurasa wa Instagram Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya. Ray C ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram dakika chache zilizopita kuwa ”rayc1982 Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasis yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za madawa ya kulevya,nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine!!roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!!namshukuru Mungu Asubuhi ya juzi Nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari Kikiwa Msaada,nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply Mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee,nikampigia akaniambia doren Hali yake si Nzuri kutokana na drugs,moyoni nikawa Nafikiria Huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!!ikawa Kama bahati,tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha madawa Mwananyamala!nilipomuona Doren Kwa Mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo,ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza Tiba ya methadone isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu Nimechoka Maisha ya utumwa nisaidie!!hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia Kwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!!am soooo happy Doren ameanza Tiba ya methadone!!!wapenzi wote wa bongo flava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye Tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa shetani.God We Trust!!!I love You my lil sister…..Nawahamasisha wengine huko Mliko mwenye ndugu,Jamaa au rafiki,njoo Katika taasis yetu uweze
Previous
Next Post »