MWANAFUNZI AUA WATU SITA KWA WAKATI MMOJA, NI MTOTO WA MTAYARISHAJI MAARUFU WA FILAMU


muuaji


muuaji2
 
Polisi nchini Marekani wamethibitisha kuwa kijana Elliot Rodger mwenye miaka 22 ambaye ni mtoto wa mtengeneza filamu maarufu, ndie aliyefanya mauaji ya watu sita kwa pamoja jijini Califonia.

Kijana huyo ambaye ni mwanafunzi ni mtoto wa Peter Rodger ambaye ni mtayarishaji filamu wa Marekani aliyesaidia kutengeneza filamu ya The Hunger Games.
Polisi wamesema kuwa kijana huyo aliwachoma visu wanafunzi watatu aliokuwa akishare nao chumba kwenye nyumba yake ambapo baadae alikwenda katika duka moja na kuanza kurusha risasi mfululizo zilizojeruhi watu na kusababisha vifo.
Baada ya tukio la kurushiana risasi na polisi Rodger alikutwa amekufa ndani ya gari lake lililopata ajali akiwa na majeraha kadhaa ya risasi kichwani.
Previous
Next Post »