Nigeria yasema iko tayari kuzungumza na Boko Haram

Nigeria yasema iko tayari kuzungumza na Boko Haram


Photo: Nigeria imesema iko tayari kuzungumza na kundi la Boko Haram kwa lengo la kumaliza mashambulizi yenye umwagaji damu yanayofanywa na kundi hilo.
Nigeria imesema iko tayari kuzungumza na kundi la Boko Haram kwa lengo la kumaliza mashambulizi yenye umwagaji damu yanayofanywa na kundi hilo.Serikali ya Nigeria imesema iko tayari kufanya mazungumzo na wanamgambowa Boko Haram ili kuokoa maisha ya wanafunzi wa kike zaidi ya 200 wanaoendelea kushikiliwa mateka na wanamgambo hao. Waziri wa Kazi Maalum, Tanimu Turaki, amesema kadhia ya kutekwa nyara wanafunzi hao mwezi uliopita imekuwa ikiikosesha usingizi serikali ya Rais Goodluck Jonathan kutokana na mashinikizo ya kila kona kutoka ndani na nje ya Nigeria. Turaki amesema serikali imewahi kutangaza mara kadhaa utayarifu wake wa kuzungumza na Boko Haram kuhusiana na masuala mbalimbali lakini kundi hilo limekuwa likipuuza wito huo wa serikali.
Siku mbili zilizopita, kundi la Boko Haram lilitoa picha ya video inayowaonyesha zaidi ya wasichana 100 wanaodaiwa kuwa sehemu ya wale 276 waliotekwa nyara na kundi hilo Aprili 14 katika eneo la Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alisema kwenye video hiyo kwamba wasichana hao hawatoachiwa huru hadi pale serikali itakapowaachia huru wapiganaji wote wa kundi lake walioko kwenye magereza ya Nigeria. Serikali ya Abuja imesema haiwezi kutekeleza sharti hilo.

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng