TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.05.2014.
Ø
MWANAMKE MMOJA
ATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA
KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
Ø
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA
MARUFUKU.
TUKIO
LA KWANZA.
MWANAMKE MMOJA ATAFUTWA NA JESHI LA
POLISI KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO.
MWANAMKE MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA
WALA MAKAZI YAKE ILA ANAFAHAMIKA KWA SURA ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA
TUHUMA ZA KUIBA MTOTO MCHANGA JINSI YA KIUME AITWAE YOSIA JEROME [MIEZI MIWII] NA KWENDA NAE MAHALI KUSIKOJULIKANA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI HUKO IKUTI- SOKONI
KATA NA TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. AWALI MTOTO HUYO AKIWA KWA MAMA YAKE
MZAZI ORESTA SHABAN [24] MUUZA
MBOGAMBOGA HAPO SOKONI, MKAZI WA IKUTI, MTUHUMIWA ALIFIKA NA KUNUNUA MBOGA
KISHA KUMUAGIZA MAMA WA MTOTO AKAMNUNULIE SAMAKI WABICHI, MAMA MTOTO ALIMWACHIA
MTOTO AMSHIKIE ATAKAPOKUWA AMEENDA KUMNUNULIA SAMAKI, MAMA HUYO ALIPOONDOKA
MTUHUMIWA NAE ALITOWEKA NA MTOTO HUYO KUELEKEA KUSIKOJUULIKANA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KATIKA
UANGALIZI WA WATOTO WAO NA KUTOWAAMINI WATU WASIOWAFAHAMU NA KUWAACHIA WATOTO.
AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA
MTOTO HUYO ALIZOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE.
KATIKA
MSAKO.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 09 KUTOKANA NA MISAKO
MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. KATIKA TUKIO
LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI
HARAMU SABA WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI
BILA KIBALI. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014
MAJIRA YA SAA 14:30HRS MCHANA
HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA KATUMBA
SONGWE, TARAFA YA UNYAKYUSA,WILAYA
YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA
WALIOKAMATWA NI 1. MICHAEL SOLOMON [45] 2.ABEBE
ISAKO [24] 3.ADISE MASHONE [20] 4.ABRAHAM MANIKO [20] 5.OCEE WATINO [26] 6.ABRAHAM GANDUU [24] NA 7.GRAM GANDULE [26]. TARATIBU ZINAFANYWA
ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI. AIDHA JESHI LA POLISI LINAMTAFUTA MTU ANAYEWAHIFADHI WAHAMIAJI HAO
AMBAE JINA LAKE LINAHIFADHIWA.
KATIKA TUKIO LA PILI:. JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. DEODATUS
JOSEPH [24] MKAZI WA KIJIJI CHA MUUNGANO –GALULA NA 2.
LENATUS DAUD [35] MKAZI WA KIJIJI CHA MUUNGANO – KALOLENI WILAYA YA
CHUNYA KWA KUKUTWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI
[VIROBA] AINA YA BOSS PAKETI 86 WAKIUZA KATIKA VIBANDA VYAO VYA BIASHARA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014
MAJIRA YA SAA 10:30HRS ASUBUHI NA SAA
15:00HRS ALASIRI KATIKA VIJIJI VYA KALOLENI NA MUUNGANO WILAYA YA CHUNYA.
KATIKA
TUKIO LA TATU:JESHI LA POLISI
LIMEMKAMATA ARON KEYELA [31] MKAZI
WA KIJIJI CHA MWASHOMA AKIWA NA PIKIPIKI MOJA T.397 BUV AINA YA T-BETTER
RANGI NYEKUNDU MALI INAYODHANIWA KUWA YA
WIZI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014
MAJIRA YA SAA 15:00HRS ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MWASHOMA, KATA YA IJOMBE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
AIDHA KATIKA MISAKO MINGINE ILIYOFANYIKA JESHI LA POLISI LIMEFANIKIWA KUKAMATA MICHE
YA BHANGI 100 IKIWA SHAMBANI PAMOJA
NA SHAMBA MOJA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA
ROBO HEKTA.
TUKIO
HILO LIMETOKEA TAREHE 14.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI
CHA ITAMBOLEO TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA
MBARALI. HATA HIVYO WATUHUMIWA WANAOMILIKI MASHAMBA HAYO WALIKIMBIA
BAADA YA KUWAONA ASKARI WA DORIA NA BHANGI HIYO IMEVUNWA NA KUHARIBIWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI YA
DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA
SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE MARA
MOJA.
Signed by
[ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon