MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA



YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 04.05.2014.

·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.

·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.939 ANC AINA YA TOYOTA MARK II ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.101 CRS AINA YA DAYUNI AITWAYE ERASTO DAUDI (23) MKAZI WA PAMBOGO NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA WA PIKIPIKI HIYO AITWAYE NATHANIEL VITUS (23) MKAZI WA PAMBOGO NA MAJERAHA KWA DEREVA WA PIKIPIKI HIYO.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:30 HUKO ENEO LA SOWETO, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA KULITELEKEZA GARI ENEO HILO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MSAKO:
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.YOHANA FAUSTINE (21) NA 2. SHABANI MSEWA (20) WOTE WAKAZI WA UHAMILA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI KETE 09 SAWA NA UZITO WA GRAMU 45.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:40 JIONI HUKO KATIKA KITUO CHA POLISI RUJEWA, TARAFA YA RUJEWA,   WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. AWALI WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KWA KOSA LA KUINGIA HIFADHI YA TAIFA IKONGA BILA KIBALI NA WAKATI WANAPEKULIWA KABLA YA KUINGIA MAHABUSU WALIKUTWA WAKIWA NA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
                                                       Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »