Mmoja wa majeruhi wa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutengenezwa ‘kienyeji’ ambao ulilipuka katika vyumba vya Hosteli za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), mtaa wa Gana jana usiku.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, amesema mlipuko unaodaiwa kutokea jana, ulitokana na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutengenezwa ‘kienyeji’ ambao ulilipuka katika vyumba vya Hosteli za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T), mtaa wa Gana
.
Amesema tukio hilo limetokea jana Jumatatu Mei 5, 2014 saa mbili usiku, na kujeruhi mtu mmoja ambaye hadi sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini humo.
Taarifa za awali kuhusu tukio hilo, zinaonyesha kuna watu/mtu ambao waliweka bomu hilo katika hosteli hizo na kupelekea tukio hilo, ambapo hadi sasa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
EmoticonEmoticon