HII NDIO STORY KAMILI : CHID BENZ AMPIGA NGWEA NA CHUPA KICHWANI USIKU WA KUAMKIA JANA.


 
Rapper Chidi Benz, amempiga Cow Bama a,k,a Ngwea nje ya Ambassador Lounge ikiyoko Mkapa tower, posta, usiku wa kuamkia leo.ugomvi huo ulitokea baada ya Chidi kumzingua Dully alipokua akiingia, ambapo mwisho wake aliamua kuondoka.

Baada ya Dully kuondoka, Ngwea aliamua kumuuliza Chidi (ambae mara nyingi huitana Dogo lao), inakuaje unamzingua kubwa lao, ndipo Chidi alipopaniki na kuanza kutoa lugha chafu huku akitaka kutokumsikiliza Ngwea, inasemekana Ngwea aliamua kukaa kimya lakini Chidi aliendelea kungea kwa hasaira na kusema "ndio nimemzingua kwani yeye nani" na kumbadilikia Ngwea ambae pia aliamua kuachana nae na kurudi ndani kwenye meza aliyokua amekaa na washkaji zake,
haikuishia hapo Chidi amkamfata kwenye meza hiyo na kuanza kumuongelea mbaya Ngwea, na ndipo Ngwea akaamua kushuka chini ya jengo kwa nia ya kuondoka. akiwa huko huko chini Chidi alimfata na kumpiga, ikiwa ni pamoja na kumkata na chupa mkononi,na kupelekwa hospitali ambapo alitibiwa.
DJ Fetty akiongea na Ngwea ambae anasema haoni chochote kilichomfanya kupigwa na msanii huyo.
Ngwea kwa sasa yupo katika kituo cha polisi Oystabay kwa ajili ya kumfungua mashtaka, licha ya kuumizwa pia ni kutokana na vitisho alivyopewa na Benzi.
Sio mara ya kwanza kwa Chidi kupiga wasanii wenzake, kama unakumbuka alishawahi kumpiga Matonya na wengine kadhaa.
Source : Djfetty
Previous
Next Post »