KWELI kifo hakina huruma! Msemo huu umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana (38) kilichotokea akiwa njiani kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.Kuambiana aliugua ghafla kwenye kambi ya kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar.Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ alisema muda mchache kabla ya kufikwa na mauti, Kuambiana alimlalamikia maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa akiendesha damu tupu.
Q-Chillah alisema:
Kwa mujibu wa watu wa karibu, Kuambiana kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo (ulcers). Lakini pia inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na kisukari (diabetes).
Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (aliomba jina kuhifadhiwa)alisema:
Q-Chilla ambaye ni miongoni wa wasanii wanaocheza filamu hiyo, aliendelea kusema kuwa siku chache kabla ya kifo, Kuambiana alimwambia filamu yake hiyo inayoitwa Jojo ndiyo ya mwisho, hatajishughulisha tena na sanaa na alikuwa na mpango wa kwenda China kupumzika kwa muda mrefu.
alisema Q-Chillah.
Habari zaidi zinasema kwamba, Kuambiana ameaga dunia hata arobaini ya mdogo wake wa damu, Patrick haijafika. Patrick alifariki dunia mwezi mmoja uliopita.
Baada ya taarifa kuenea, wasanii mbalimbali wa filamu walikusanyika katika Hospitali ya Mama Ngoma ambapo Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ walivunja rekodi ya kulia kufuatia kifo hicho.
Wadau na mashabiki wa filamu waliokuwa eneo hilo walisikika wakisema kwamba wasanii wengi hawana tabia za kucheki afya zao, jambo ambalo linawagharimu kiasi cha kupoteza maisha.
Wengine walisikika wakisema kwamba watu wanaoanguka chooni mara nyingi huwa hawaponi, wakipona huwa wanapooza miili.
Unajua watu wengi wanakosea, pale mtu anapodondoka chooni wanamkimbiza hospitali badala ya kumtibu kienyeji, mtu akianguka chooni tu anatakiwa kupewa ndizi mbivu lakini akipelekwa hospitali lazima afe
walisikika watu.
Marehemu Kuambiana alizaliwa mwaka 1976, Ifunda mkoani Iringa. Kabila ni Mmakua wa mkoani Mtwara.
EmoticonEmoticon