Ujumbe wa Swebbe kwa Kanumba


Msanii wa filamu aliyetamba na kundi la Kaole Sanaa Group, Swebe Santana amekuwa miongoni mwa wasanii wa filamu walioandika ujumbe maalum kwa marehemu Kanumba ikiwa leo anatimiza miaka miwili tangu afariki dunia.
Swebbe ameandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa herufi kubwa akionesha hisia zake na mtazamo wake kuhusu tasnia ya filamu na kinachoendelea.
“Kwa sasa filamu zinauzwa kwa majina na sura na si uwezo…yote kwa yote soko la filamu limekufa Bongo..” Inasomeka sehemu ya ujumbe mrefu wa Swebbe.
Swebbe amedai kuwa ana mengi ya kumwambia Kanumba lakini anaomba Mungu amsamehe huku akiwarushia dongo wale aliodai wanafanya dhihaka kwa kutumia jina lake.
“Zangu dua zitakufikia na Mungu mwenye sifa ya kusamehe akusamehe..na wanaofanya dhihaka juu ya hilo nao awasamehe. Hakika kwa Mungu wote tutarejea…nina mengi..lakini kwa haya machache wacha tuu nijifute chozi na dua kukuombea…R.I.P rafiki yangu mpendwa Steven Charles Kanumba.”
Previous
Next Post »