TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 30.04.2014.




Ø  MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI BARABARANI.

Ø  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA BHANGI.

Ø  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA  LIMEKAMATA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA  NYATI.

TUKIO LA KWANZA.

GARI  NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ISAKA SHEDRACK [20] MKAZI WA SAE JIJINI MBEYA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 29.04.2014 MAJIRA YA  SAA 19:30 JIONI KATIKA ENEO LA MAMA JOHN, KATA YA  MWAKIBETE,TARAFA YA  IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA  AJALI  HIYO BADO KINACHUNGUZWA NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.  AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [DEREVA] AZITOE  KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

KATIKA MSAKO.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA BHANGI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI. KATIKA TUKIO LA KWANZA JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA VICTOR GEORGE [38] MKAZI WA KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA  BAADA YA  KUKAMATWA AKIWA NA KETE 15 ZA BHANGI ZENYE UZITO WA GRAM 75.

MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA  TAREHE 29.04.2014 MAJIRA YA  SAA 12:50 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUPA, KATA YA  LUPA,TARAFA YA  KIPEMBAWE. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI KUMFIKISHA MAHAKAMANI.

KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA  LINAMSHIKILIA MANENO MASARU [25]  MKAZI WA KIJIJI CHA MADABAGA WILAYA YA  MBARALI  BAADA YA  KUKAMATWA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA KILO 15. PIA MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA NA BAISKELI TATU [03] AINA YA BAMBUCHA MALI INAYODHANIWA KUWA NI YA  WIZI.

MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA TAREHE  29.04.2014 MAJIRA YA  SAA 15:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MADABAGA, KATA YA  CHIMALA, TARAFA YA  RUJEWA, WILAYA YA  MBARALI. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI KUMFIKISHA MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA  JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA MATUMIZI  YA  DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

AIDHA KATIKA TUKIO JINGINE LA MSAKO JESHI  LA POLISI MKOA WA MBEYA  LIMEKAMATA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA  NYATI.KATIKA TUKIO HILO JESHI LA POLISI LILIKAMATA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA  NYATI YENYE UZITO WA KILO 300 IKIWA INASAFIRISHWA KWA KUTUMIA PIKIPIKI T. 494 CDF AINA YA  T-BETTER.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 29.04.2014 MAJIRA YA SAA 15:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGAWA, KATA YA  LUGELELE,TARAFA YA  RUJEWA WILAYA YA  MBARALI KATIKA BARABARA KUU YA  MBEYA/NJOMBE. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KUITELEKEZA PIKIPIKI YAKE MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI WA DORIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA  JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZILIZOPO KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE  KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »