·
MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA
NA PIKIPIKI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA KWA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE 24.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WAHAMIAJI HARAMU WATATU RAIA WA NCHINI ETHIOPIA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WANNE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA BHANGI
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MPANDA BAISKELI
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MAIKO
PETER (45) MKAZI WA KAFUNDO
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.361 CRS AINA YA SANLG ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA WAKILI
MWASUNGUTI.
AJALI HIYO
ILITOKEA MNAMO TAREHE 02.04.2014
MAJIRA YA SAA 19:15 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA KAFUNDO, KATA YA IPINDA, TARAFA YA NTEBELA WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KUITELEKEZA PIKIPIKI MARA BAADA YA AJALI.
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJAI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA
WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMOS CHARLES (32) MFUGAJI, MKAZI WA MAMBA F KWA TUHUMA ZA WIZI WA NG’OMBE
WAPATAO 24 MALI YA MFUGAJI AITWAYE BUNDALA
MSOMA (64) MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA F.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.03.2014
MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO
KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. THAMANI HALISI YA NG’OMBE HAO NI TSHS. 7,200,000/=. CHANZO NI KULIPIZA KISASI BAADA YA MTUHUMIWA
KUMDHAMINI MAHAKAMANI MTOTO WA MLALAMIKAJI LEA
MASASI ALIYEKUWA ANAKABILIWA NA KESI YA KUFANYA FUJO KISHA KUTOROKA.
MTUHUMIWA KABLA
YA KUTEKELEZA UHALIFU HUO ALIVUNJA ZIZI LA NG’OMBE NA KISHA KUIBA. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA AKIWA NA NG’OMBE 23
NYUMBANI KWAKE. MARA UCHUNGUZI UTAKAPO KAMILI ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHANA NA TAMAA YA MALI NA BADALA YAKE WATUMIE NJIA HALALI KUJIPATIA KIPATO.
AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTUMIA NJIA ZA AMANI KWA KUKAA MEZA MOJA YA
MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA WA MIGOGORO YAO.
KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WATATU WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA
NCHINI BILA KIBALI. WAHAMIAJI HAO HARAMU NI 1. ABRI KABAI (26) 2. KISHETI KIBANO (21) NA 3. CHIKAMLA GEORGE
(24) WOTE WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA.
WAHAMIAJI HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.04.2014
MAJIRA YA SAA 05:30 ALFAJIRI KATIKA
ENEO LA STENDI KUU, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU
ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PALE WANAPOWAONA WATU WANAOWATILIA MASHAKA
KATIKA MAENEO YAO ILI WAFANYIWE UCHUNGUZI/UPELELEZI. AIDHA ANATOA WITO KWA
WAGENI/WAHAMIAJI KUFUATA TARATIBU/SHERIA ZA UHAMIAJI IKIWA NI PAMOJA NA KUWA NA
KIBALI KINACHOWARUHUSU KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA USUMBUFU.
KATIKA MISAKO ILIYOFANYIKA:
KATIKA MSAKO WA
KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE 1. ALOYCE
ALFRED (22) 2. ABEL MTAWA (19)
3. AWAMI HARUNA (23) NA 4. KENETH KIZITO (30) WOTE WAKAZI WA MBALIZI WAKIWA NA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA
TATU [03].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA
MNAMO TAREHE 03.04.2014 MAJIRA YA
SAA 11:30 ASUBUHI KATIKA ENEO LA
MBALIZI, KATA YA UTENGULE –USONGWE, TARAFA YA BONDE LA SONGWE WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA
PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA FRANK MWAKIKAO (26)
MKAZI WA ILOLO AKIWA NA BHANGI KETE 10
SAWA NA UZITO WA GRAM 50.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.04.2014
MAJIRA YA SAA 11:55 ASUBUHI HUKO
KATIKA MTAA WA MAKUNGULU, KATA YA MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] NA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon