PICHA YA RAIS OBAMA NA ORTIZ YAZUA KIZAAZAA


Rais Obama akipiga picha na David Ortiz.
IKULU ya Marekani imeikashifu kampuni ya simu ya Samsung kwa kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyopiga na mchezaji maarufu nchini Marekani David Ortiz kama tangazo la kibiashara.
Rais Obama akiwa na jezi yake baada ya kukabidhiwa na Ortiz.
Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki.
Hata hivyo kampuni ya Samsung iliisambaza kupitia kwa mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.
Msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara.
Wakuu wa Samsung hawajasema lolote kuhusu malalamiko ya White House.
Bwana Carney amesema kuwa mawakili wa White House wanashauriwa kuhusu kitendo hicho cha Samsung.
Picha ya Obama na Ortiz baada ya kuwekwa kwenye ukurasa wa Samsung katika mtandao wa Twitter.
"Bila ya kusema mambo mengi, nataka niwaambie tu kwamba White House inapinga vikali jambo hili,'' alisema Carney
Ortiz alimpa Rais Obama jezi maalum kutoka kwa klabu anayochezea ya Red Sox ikiwa na jina la Rais siku ya Jumanne na kisha kumshawishi kujipiga naye picha mwenyewe inayojulikana kama 'Selfie'.
"Nilimpa jezi na wapiga picha wakatupiga picha, basi nilijhisi na mimi kujipiga naye picha'' alisema mchezaji huyo.
Alikana kuwa kampuni ya Samsung ilimlipa pesa kwa picha hio.
Chanzo: BBCSWAHILI
Previous
Next Post »