MTU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 19.04.2014.


·         MTU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WATU WASIOFAHAMIKA.
  
·         MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
  
·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.
  
KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 30-35 ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA KWENYE KORONGO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.04.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ITAKA, KIJIJI CHA ICHENJEZYA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO CHA TUKIO HILI BADO KINACHUNGUZWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA  KIUME MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 30- 35 ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA JINA NA MAKAZI YA DEREVA WAKE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.04.2014 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA MTAA WA MWAKAPANGALA, KIJIJI CHA MWASHIWAWALA, KATA YA UTENGULE /USONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJNI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.

CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.


KATIKA MISAKO:

WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ABRAHAM MPONGWE (37) NA 2. MONISLITA MAPUNDA (18) WOTE WAKAZI WA CHIANGA – NAKONDE ZAMBIA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI KETE 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.04.2014 MAJIRA YA SAA 11:40 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA MTAA WA MWAKA-TUNDUMA   KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »