TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI.“PRESS RELEASE” TAREHE 16. 05. 2013

 

 

 

 
 
 

WILAYA YA MBARALI - MAUAJI

MNAMO TAREHE 15.05.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MADIBILA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA . FAUSTINO S/O LULAMBO,MIAKA 55,MBENA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA KANAMALENGA- MKUNYWA ALIUAWA KWA KUKATWA MUNDU KICHWANI NA MKONO WA KUSHOTO NA ISRAEL S/O MKULA,MIAKA 20,MBENA MKULIMA MKAZI WA ILUNDA MTWANGO MKOA WA NJOMBE. AIDHA KATIKA TUKIO HILO EMANUEL S/O MLAGALA,MIAKA 28,MBENA,MKULIMA MKAZI WA MUFINDI AMBAYE ALIKUWA NA MAREHEMU  ALIJERUHIWA KWA KUKATWA MUNDU KICHWANI-KISOGONI NA MIKONO YOTE MIWILI . CHANZO NI UGOMVI ULIOTOKEA KATIKA MASHAMBA YA MPUNGA  KATI YA MTUHUMIWA NA EMANUEL S/O MLAGALA AMBAYE ALIKUWA AKIMTUHUMU MTUHUMIWA  KUMUIBIA SIMU YAKE NA  MAREHEMU AKIWA NA MUNDU MKONONI ALIKWENDA KUAMUA UGOMVI HUO NDIPO MTUHUMIWA ALIPOMNYANG’ANYA MUNDU NA KUANZA KUWASHAMBULIA . MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA MADIBILA NA MAJERUHI AMELAZWA KATIKA KITUO HICHO CHA AFYA . MTUHUMIWA AMBAYE PIA ALIPATA MAJERAHA NA KUTIBIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

 

WILAYA YA MBEYA - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU KUPINDUKA

                                     NA KUSABABISHA KIFO.

 

MNAMO TAREHE 15.05.2015 MAJIRA YA SAA 00:30HRS HUKO ENEO LA ILOMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.332 ASV AINA YA TOYOTA CARINA LIKIENDESHWA NA ASKARI POLISI NOVATUS, MIAKA 39,MFIPA  WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WILAYA YA MBEYA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA MWANAUME UMRI KATI YA MIAKA 25-30 NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA MOMBA - KUCHOMA NYUMBA MOTO

MNAMO TAREHE 15.05.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NAMALE WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. FARAHIWELU S/O SINKALA,MIAKA 52,MNYAMWANGA,MKULIMA ,MKAZI WA KIJIJI CHA NAMOLE ALICHOMEWA NYUMBA YAKE YA KUISHI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. NYUMBA HIYO YA VYUMBA VIWILI IMEJENGWA KWA KUTUMIA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA NYASI. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA NA ILIYOOKOLEWA BADO KUJULIKANA. CHANZO NI TUHUMA ZA UCHAWI BAADA YA MHANGA KUTUHUMIWA KUWA NI MCHAWI HAPO KIJIJINI KWA KUMLOGA JIRANI YAKE AITWAE MAMA NAMKAMBA ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 14.05.2013. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOSADIKI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO. MSAKO UNAENDELEA KUFANYWA ILI KUWAKAMATA WATUHUMIWA WOTE.

WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

MNAMO TAREHE 15.05.2013 MAJIRA YA SAA 21:30HRS HUKO ISANGA STENDI YA CHUNYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA JOSEPH S/O NGANDEKULA,MIAKA 44,MKULIMA MRUNDI RAIA WA BURUNDI AKIWA NA WENZAKE 17 WOTE RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI .MBINU ILIYOTUMIKA NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO . WATUHUMIWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KUHUSU WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA RAIA WA KIGENI ILI HATUA DHIDI YAO ZICHUKULIWE. 

Signed By

 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

 

 

 

Previous
Next Post »