picha ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo, katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo.
Mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm
katibu wa vijana wilaya ya arumeru akiwa Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa chadema.
Jumla ya wananchi 100 wa kata ya Ortumunti wilayani Arumeru kutoka katika vyama mbalimbali vya upinzani wamehamia chama cha Mapinduzi akiwemo mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA wa kata hiyo .
tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki,wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika kijiji cha Elikiushing kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.
Akiongea wakati wa kurudisha kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya CCM,Mwenyekiti wa vijana wa CHADEMA, Thomasi Molel alisema kuwa ameamua kuchukuwa hatua hiyo mara baada ya kubaini kuwa tangu awe mfuasi wa cha hicho (CHADEMA),Hajapata faida yoyote wala hajaona kitu ambacho wananchi wanafaidika kupitia chama hicho.
Alisema kuwa yeye ni mwanasiasa mzoefu kwani alianza kuingia katika siasa tangu mwaka 1995 na anajua siasa vilivyo, hivyo ameamua kuondoka katika chama hicho kwani CHADEMA ni chama ambacho hakina demokrasia ya kweli ambayo inatakiwa iwenacho kama chama
Alisema kuwa viongozi wengi wa CHADEMA wamekuwa wanatoa ahadi za uongo kwa wananchi na mbali ya hivyo pia chama hicho kimekuwa na wasemaji wengi kwani kila kiongozi amekuwa anasema anachotaka badala ya kuwa na msemaji mmoja ambaye ndie atakaeweza kukisemea chama .
Aidha alibainisha kuwa katika kata yao tangu upinzani wameingia madarakani hamna kitu ambacho wamewafanyia wananchi badala yake wamekuwa wakiwachangisha wananchi hela nyingi bila kufanya maendeleo yeyote akitolea mfano mchongo wa shilingi elfu mbili ambao ulichangishwa kwa kila mwananchi wa kike na kiume ikisemekana ela hiyo ingeweza kujengea shule lakini adi leo hela hile aijafanya chochote na aijulikani ilipopelekwa
Aliongeza kuwa kingine ni kile kitendo cha kutosomewa mapato na matumizi ya kata yao tofauti na kipindi ambacho ccm ilikuwa madarakani hivyo.
Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Arumeru Godfrey Sabuni alisema kuwa wao kama ccm wanawaapokea wananchama hao na pia wamesikia baadhi ya matatizo yao likiwemo la kutosomewa bajeti ya mapato na matumizi kwa kipindi kirefu na aliwaaidi kufuatilia swala hili kwa kwenda katika ofisi ya mkurugenzi kufuatilia swala hili.
Aliwasihi wananchi kutofanya makosa katika kipindi hichi kunakoelekea uchaguzi mdogo wa viongozi wa vijiji na vitongoji kwani wakifanya kosa kwa kuchagua viongozi wabovu wataendelea kuteseka na kata yao haitapata viongozi wazuri.
EmoticonEmoticon