MBARONI KWA KUMCHOMA BISIBISI MAMA YAKE MZAZI

Bi Habiba Said au Mama Nyamsati aliyejeruhiwa kwa bisibisi na kijana wake wa kumzaa anayefahamika kwa jina moja la Jumanne(28) .

Stori: hande Abdallah na Denis Mtima 
jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Jumanne (28), ametiwa mbaroni na polisi kwa kosa la kumchoma kwa bisibisi mama’ke mzazi aitwaye Habiba Said au Mama Nyamsati na kumsababishia majeraha makubwa kichwani.
 Tukio hilo la kusikitisha lilijiri hivi karibuni, maeneo ya Temeke-Pire jijini Dar ambapo Jumanne alidaiwa kutenda unyama huo kwa kumshambulia mama’ke kwa fimbo kisha kuchukua bisibisi na kumchoma nayo kichwani kwa madai kuwa anataka kurudi jela akale ugali wa bure.
kijana Jumanne(28) akitiwa nguvuni.

 Ilidaiwa kuwa baada ya wadogo zake Jumanne kumuona kaka yao akidhamiria kumuumiza mama yao ndipo wakaingilia kati ili kumzuia, lakini Jumanne aliwapiga wote na kumjeruhi mdogo wake mwingine kwa bisibisi hiyohiyo.
Raia wakimshangaa kijana Jumanne kwa kitendo alichofanya kwa mama yake mzazi.

 Wakati tukio hilo likiendelea, majirani na ndugu walikwenda kutoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Wailes, Temeke ambapo polisi walifika eneo hilo na kumkamata Jumanne huku mama yake akipatiwa PF-3 kwa ajili ya matibabu katika Hospitali ya Temeke. Baadaye mtuhumiwa huyo alihamishiwa Kituo cha Polisi Chang’ombe.

 Ilifahamika kwamba mama huyo alishonwa nyuzi kadhaa kichwani baada ya kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na wanahabari wetu, mama huyo alisema kuwa siyo mara ya kwanza kwa mwanaye kumshambulia kama hivyo kwani aliwahi kumshambulia kwa kumpiga vichwa bila kujali kama alikuwa na mtoto mdogo mgongoni ambaye ni mdogo wake Jumanne.


 “Huko nyuma alishawahi kunivamia nikiwa na huyu mdogo wake mgongoni akanipiga vichwa hadi uso wote ukavimba,” alisema mama mzazi wa Jumanne na kuongeza:
 “Nilisimama naye mahakamani na akafungwa miezi 6 kisha akaachiwa.”

Mzazi huyo alisimulia kwamba chanzo cha mwanaye kuwa katika hali hiyo inawezekana ni mambo ya Kiswahili (kulogwa) kwa sababu siyo kawaida kwa mtoto kumpiga mama’ke.


 Baada ya soo hilo kufikishwa kituoni hapo, shitaka hilo lilifunguliwa jalada ya CH/RB/2975/14 KUJERUHI ambapo polisi wanaendelea na uchunguzi ili jamaa afikishwe mahakamani.
SOURCE:GPL
Previous
Next Post »