MAAJABU YA MUNGU


Paul Ngido na Asha Yahya  wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali waliowazaa watoto Keisha na Glory.

KATIKA hali ya kushangaza, wagonjwa wa mtindio wa ubongo, Paul Ngido na Asha Yahya wanaolelewa kwenye kituo cha watoto wenye matatizo mbalimbali wakiwemo yatima cha Ngido kilichopo Mazimbu FK mkoani hapa wamejikuta wakizaa watoto wawili, Keisha na Glory ndani ya kituo hicho.Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho, Linda Cyprian Ngido amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye kituo chake na kusema kwamba huo nao ni msalaba anaotakiwa kuubeba.
Uwazi lilimuuliza mkurugenzi huyo kwa nini wazazi hao wasiruhusiwe kubariki ndoa na kuishi kama mume na mke, alijibu:


Paul Ngido na Asha Yahya wanaodaiwa kuwa na mtindio wa ubungo wakiwa na watoto wao wawili waliozaa ndani ya kituo hicho, Keisha na Glory.

“Niliwahi kuongea na mchungaji kuhusu hilo, lakini akakataa akidai hawezi kufungisha ndoa ya watu wenye upungufu wa akili.“Kama wewe (mwandishi) utanisaidia kufanikisha jambo hilo nitashukuru sana,” alisema mkurugenzi huyo.
Baada ya majibu hayo  mwandishi wetu alikwenda kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ‘KKKT’ Dayosisi ya Morogoro na kuonana na Askofu Jacon Mameo. Aliulizwa kuhusu wazazi hao, akasema:
“Kwanza taarifa hizo nzito ndiyo nazisikia kwako. Huyo mchungaji alifanya makosa, neno ndoa ni muungano wa watu wawili, mwanamke na mwanaume hivyo kama watu wameungana na kufanikiwa kuzaa watoto na kuwalea vizuri hao wana akili timamu, tena wako kwenye uangalizi wa kituo, labda kipingamizi kiwe kwa wazazi kwani ndoa haiwezi kufungwa kama wao hawajakubali,” alisema askofu huyo.
Mwandishi wetu alirudi tena kweye kituo hicho na kuzungumza na familia hiyo. Wa  kwanza alikuwa Paul ambapo alisema: “Mimi wazazi wangu siwajui, mama yangu ni huyu (mkurugenzi wa kituo) na ndiyo maana amenipa majina mapya”.
Kwa upande wake, Asha alipoulizwa kama wazazi wake wameridhia kubadili dini na kufunga ndoa ya  Kikristo na Paul alisema: “Ndiyo.”
Mwandishi wa habari hii atabeba jukumu la kutoa sehemu ya mahari hiyo ili wawili hao wafunge ndoa lakini mpaka pale wataalam watakapothibitisha kwamba sasa wazazi hao wako fiti kiakili (anafuatilia).
Kituo hicho kina watoto na watu wazima 53 wenye matataizo ya mtindio wa ubongo, watoto 10 waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu, baadhi yao wakiwa yatima.

SORCE: GPL
Previous
Next Post »