Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya |
Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo. |
Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu |
Kufuatia kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya kampuni ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga marufuku mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si salama kwa wasafiri na wapita njia.
Wananchi hao ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la Ipuli mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda shuleni kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la A.M Coach lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.
Aidha wananchi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya kampuni hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana kuyumba barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu za mkoa wa Tabora.
Wameitahadharisha Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima.
EmoticonEmoticon