DEREVA WA BODABODA AUAWA NA MWILI WAKE KUTELEKEZWA PORINI.





TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 10.04.2014.


DEREVA WA BODABODA AUAWA NA MWILI WAKE KUTELEKEZWA PORINI.

MTU ALIYETAMBULIWA KWA JINA LA SIZA JOHN @ MWAMBENJA, {28} DEREVA BODABODA, MKAZI WA AIRPORT ALIKUTWA AMEUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA PORINI.

TUKIO HILO LILITOKEA KATIKA ENEO LA SENJELE – IYELA KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA  MKOA WA MBEYA AMBAPO MAREHEMU ALIONEKANA MARA YA  MWISHO TAREHE 08.04.2014 MAJIRA YA JIONI AKIWA KATIKA KIJIWE CHAKE AIRPORT – MADINI NA PIKIPIKI YAKE T.932 CTZ AINA YA  KINGLION NA ALIONDOKA NA MTEJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA HADI ALIPOKUTWA AKIWA AMEUAWA NA MWILI WAKE KUTUPWA PORINI KANDO YA  RELI YA  TAZARA UKIWA  UMETAPAKAA DAMU NA MAJERAHA MAENEO MBALIMBALI YA MWILI WAKE NA PIKIPIKI IKIWA  IMETELEKEZWA UMBALI WA MITA 13.

CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MUANDAMIZI WA POLISI AHMEDI MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI MTUHUMIWA AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA PIKIPIKI.

MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE SAFELI MWAKANSOPE, [60] MKAZI WA KIJIJI CHA LUBELE KATA YA IKIMBA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA  KYELA MKOA WA MBEYA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.416 CGE AINA YA  SANLG IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.

AJALI HIYO IMETOKEA KATIKA BARABARA YA KASUMULU/TUKUYU MNAMO TAREHE 08.04.2014 MAJIRA 19:00 JIONI. DEREVA WA PIKIPIKI ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MUANDAMIZI WA POLISI AHMEDI MSANGI ANATOA WITO KWA MADERA WA VYOMBO VYA MOTO KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI PIA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA DEREVA HUHYO AZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI MTUHUMIWA AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.

TUKIO HILO LILITOKEA HUKO KATIKA ENEO LA MAPELELE- MBALIZI, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIWAKAMATA 1. JOHN THOMAS, [23] NA 2. HUSSEIN JUMA, [24] WOTE WAKAZI WA MBALIZI  WAKIWA NA BHANGI  KETE 21 SAWA NA UZITO WA GRAM 105. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.




Signed by:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]

Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »